Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, June 30, 2013

LUCY CHARLES ATWAA UMALKIA WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013

Mrembo Lucy Charles akitabasamu baada ya kuvikwa taji la Redd's miss Kanda ya Ziwa usiku huu.

Kinyanganyiro cha kumtafuta mnyange wa Kanda ya Ziwa kwa mwaka 2013, kimeteguliwa usiku huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest baada ya Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo wengine 17 waliojitokeza.

Mrembo huyo aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa Hotel ya Gold Crest baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza Ni changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Eshe Rashid  na mshindi wa tatu ni Salsha Isdore

Vinara watatu .katikati ni Lucy Charles mshindi wa Redd's miss Lake zone 2013, kulia ni Eshe Rashid kutoka Mara na kushoto ni Salsha Isdore kutoka Geita na wote watatu wanaenda ngazi ya taifa.
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Yussuf Makamba(kushoto) na kulia ni Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula wakiwa ni wageni rasmi

Furaha ikitanda kwa kila mmoja
Hapa kila mmoja alikuwa na wake wa kumchangua na kila mmoja akijiuliza swali nani kutwaa taji !!
Jamal Kalumuna kutoka Bukoba akiwa na furaha baada ya kuwaona warembo jukwaanin
Meza kuu Viongozi mbalimbali
Mwandaaji wa Miss Redd's Lake Zone 2013 akisikiliza neno kutoka kwa  Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga
Mc Kulia akiwa na Mwandaaji ambaye anahusika na Swala zima na akiwa anatoka Clara Salon & Boutique Bi Clara Mwassa.
Furaha zikapenya kwa Viongozi hawa ambao ndiyo walikuwa majaji
Umati wa watu ukimwangalia kwa makini Mashidonge wakati anacheza na Moto usiku huu
Michuzi ikimfata alipo!!
Babylove Kalalaa akiwa na nyoka wake jukwaani kuwapagawisha mashabiki wake.
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Yussuf Makamba ilibidi asimame maana ilikuwa kazi kweli kweli na kwa mara ya kwanza namuona na yeye anachukua kumbukumbu kwenye simu yake.!!
warembo wote wakaitwa !!





Kiongozi wa BHATT ELECTONICS LTD Akiteta baada ya kuchagua warembo na kuwapatia kazi kwenye ofisi zao. Kumbuka BHATT ni wakala wa Samsung.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga akijiandaa kuanza kuita 10 Bora hapa
Top Ten hii hapa
Tano Bora

Ommy Dimpoz akitumbuiza
Dadaz wakidata na nyimbo za mkali Ommy Dimpoz
Michael Ross Kutoka Uganda nae akaingia kwa mitindo ya aina yake!!
Dadaz wakimsonga Michael Ross kutaka kumshusha chini kucheza nae




kamata kitita chako Mrembo!!!
Zawadi zako hizi!!

ushindi  mtamu jamaniiii!
Picha ya pamoja Waandaji na majaji wa Redd's miss Lake zone 2013
Wanyange !!


No comments:

Post a Comment