Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, June 30, 2013

FC VITO YA LINDI INAKWENDA FINLAND KUCHEZA HELSINKI CUP 2013

 Logo ya klabu ya FC Vito iliyo chini ya Kituo cha Michezo cha Sports Development Aid (SDA), kilicho katika Manispaa ya Lindi.
 Mkurugenzi wa SDA, Chigogolo Mohammed (wa kwanza kulia nyuma), akiwa katika picha ya pamoja nje ya ofisi za kituo hicho na baadhi ya wachezaji wa FC Vito. Kushoto nyuma ni Mratibu wa SDA, Ramson Lucas na Kocha Jamal Lisuma.
 Mkurugenzi wa SDA, Chigogolo Mohammed (wa kwanza kushoto nyuma), akiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha kwanza cha FC Vito. Kulia nyuma ni Mratibu wa SDA, Ramson Lucas na katikati ni Kocha Jamal Lisuma.
  Kocha wa FC Vito, Jamal Lisuma.
 Baadhi ya nyota wa FC Vito wakiwa katika meza ya chakula.
 Mratibu wa SDA, Ramson Lucas akiwanoa yoso wa FC Vito alipokamata kwa muda jukumu la Kocha Jamal Lisuma ambaye ndiye kocha wa kikosi hiki.
 Wazazi na walezi wa vijana wa timu ya FC Vito, wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji hao (waliovaa track-suit za bluu), katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika mjini Lindi hivi karibuni.
 Juu: Wachezaji wa FC Vito wakimsikiliza mmoja wa wageni aliyetembelea mazoezi ya kikosi hicho na kupata nafasi ya kuzungumza nao. 

DAR ES SALAAM, Tanzania

Helsinki Cup ni michuano ya wiki moja kila mwaka, ambapo mwaka huu itahusisha zaidi ya timu za vijana 860 kutoka nchi 23 duniani, zitakazoumana katika soka la vijana wa kike na kiume walio chini ya miaka 11

TIMU ya soka ya vijana ya FC Vito ya Lindi Mjini, imetua jijini Dar es Salaam, ikiwa safari kuelekea Helsinki, Finland, inakokwenda kushiriki Michuano ya Kombe la Helsinki, linalotarajia kuanza kutimua vumbi Julai 8 na kumalizika Julai 13.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Mkurugenzi wa Kituo cha Sports Development Aid (SDA), kinaichomiliki FC Vito, Mohammed Chigogola, alisema kuwa kikosi chake kinatarajia kuwa Dar es Salaam kwa siku mbili, kabla ya Jumatano kusafiri.

Aliongeza kuwa, wakiwa Dar, Jumanne wanatarajia kufanya mkutano na vyombo vya habari utakaofanyika Ubalozi wa Finland nchini, ambapo watatumia nafasi hiyo kuelezea mambo kadhaa yahusuyo safari yao hiyo.

Kwa mujibu wa Chigogola, Helsinki Cup ni michuano ya wiki moja kila mwaka, ambapo mwaka huu itahusisha zaidi ya timu za vijana 860 kutoka nchi 23 duniani, zitakazoumana katika soka la vijana wa kike na kiume walio chini ya miaka 11.

Chigogola aliongeza kuwa, msafara wa FC Vito utakuwa na jumla ya watu 15, wakiwamo viongozi watatu na wachezaji 12.

Aliwataja viongozi watakaosafiri na kikosi hicho pamoja nay eye kuwa ni Mratibu, Ramson Lucas na Kocha Mkuu Jamal Lisuma.

Akiwataja nyota waliochaguliwa kuwamo katika msafara huo, kocha Jamal Lisuma aliwataja kuwa ni  Mohammed Mussa, Osama Aman, Ramadhani Hassan, Abdul Mussa, Abdallah Mbade, Karim Bakiri, Juma Msafiri na Ashrafu Hassan.

Wengine ni pamoja na Mohammed Selemani, Hossam Hassan, Dominic William na nahodha Humphrey Lambaert. 10.

Katika mahojiano, Kocha Jamal anaenda mbali zaidi na kusema anajisikia furaha  kuwa kocha wa kikosi hicho, sio kutokana na kupata nafasi ya kusafiri, bali kwa namna viongozi wa kituo wanavyompa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Najivunia ushirikiano ninaopata katika kufanikisha program zangu. Uongozi unanisikiliza na kunipa kila ninachohitaji katika kuwezesha kikosi kuwa fiti kiakili, kimwili na kimbinu, hivyo kuwapa uwezo wa kupokea vema mafundisho yangu,” anafafanua Jamal.

No comments:

Post a Comment