LONDON, England
HATIMAYE ‘Special One’ amerudi Stamford Bridge
kufanya makubwa zaidi, hiyo ni changamoto kwake hasa kutokana na kutwaa mataji
sita katika miaka mitatu aliyokaa Chelsea kwenye utawala wake wa kwanza.
Ni vipi Jose Mourinho atafanikiwa katika hilo?
Jibu ni rahisi sana, atafanikiwa kwa kutengeneza uti
wa mgongo kwenye timu tena.
Wakati wa utawala wake wa kwanza, alikuwa na Petr
Cech golini, John Terry beki wa kati, Frank Lampard kiungo na Didier Drogba
mshambuliaji wa kati.
Hawa wote wananjaa ya ushindi, wote ni viongozi na
wote ni wachezaji wa mechi kubwa.
Hili linathibitishwa na ubingwa mara mbili wa Ligi
Kuu England, mataji mawili ya Kombe la Ligi, Kombe la FA na Ngao ya Jamii.
Na hii ndiyo sababu itakayomlazimu kutengeneza upya
uti wa mgongo wa timu hiyo.
Kikosi cha sasa cha Chelsea kinaubora wa hali ya
juu, lakini hakina ari ya ushindi, njaa ya mafanikio pamoja na jihadi kama
ilivyokuwa kwenye utawala wa kwanza wa Mourinho.
Na kufanikisha hilo anatakiwa kufanya biashara ya
kuuza wachezaji, ili apate fedha za kununua.
Mtu wa kwanza kufunguliwa milango atakuwa Fernando
Torres na kuangalia uwezekano wa kumleta Straika wa Napoli, Edinson Cavani kuja
kumaliza tatizo la magoli Chelsea.
Mourinho anahaha kutafuta mtu wa kumtazama kwenye
safu ya ushambuliaji ya Chelsea, mtu kama Cavani. Lakini pia anaweza kumchukua
Robert Lewandowski kutoka Borussia Dortmund au hata Wayne Rooney wa Manchester
United.
Bayern Munich wanapewa nafasi ya kumsajili
Lewandowski na Man United wanasema Rooney anabaki, kwa hiyo matumaini yote yapo
kwa Cavani.
Nyuma ya straika anaweza kutoa nafasi kwa utatu
mtakatifu wa Juan Mata, Eden Hazard na Oscar kufanya yao.
Maneno kwamba Mourinho si muumini wa soka la
kushambulia ni upuuzi, jamaa aliweka rekodi ya kumaliza na pointi nyingi
England na Hispania na huwezi kufanya hilo kwa kupaki basi.
Na hiyo ndio maana timu hii itakuwa kama Chelsea ya
wakati ule, iliyokuwa na vipaji vya ukweli vya Arjen Robben, Eidur Gudjohnsen
na Joe Cole.
Nyuma yao kulikuwa na Claude Makelele, kiungo bora
zaidi wa ulinzi kuwahi kutokea duniani na ufunguo wa mafanikio ya Chelsea
kwenye miaka hiyo.
Lakini muundo mpya safari hii, utashuhudia watu
wawili wakiwa na jukumu hilo, kwanza Lampard, mfungaji bora muda wote wa
Chelsea, akiwa na majukumu kama Xabi Alonso ya kuanzisha mashambulizi kutoka
chini.
Jamaa pia anaweza kupanda mbele mwenyewe na
kuendelea kucheka na nyavu, akicheza sambamba naye atakuwa Luka Modric.
Mourinho alimpeleka Real Madrid mwaka jana.
Mourinho anamuamini kiungo huyo licha ya watu
Hispania kumponda. Modric ni mmoja kati ya wachezaji wawili ambao Mreno huyo
atakuja nao Stamford Bridge, kutoka Santiago Bernabeu.
Mwingine siyo Cristiano Ronaldo, bali ni Raphael
Varane kinda wa Kifaransa mwenye miaka 20, ambaye anatabiriwa kuja kuwa mmoja
kati ya mabeki bora wa kati duniani.
Varane pia anaweza kucheza kama kiungo wa ulinzi au
mfagiaji (sweeper), lakini la kwanza kwa Mourinho ni kuwa anampenda na
kumuamini kinda huyo anapocheza kama beki. Madrid hawataki kumuuza, Special One
hataki kuelewa hilo.
Mourinho anasema anasubiri kucheza na David Luiz,
beki asiyetabirika, lakini soka la kujilipua la Mbrazil huyo litamkera Mourinho
na anaweza kumfungulia milango mapema tu.
Luiz atapata nafasi, japokuwa Terry atarudisha namba
yake, huyu ni mwanajeshi wa Mourinho tangu zamani na itaendelea kuwa hivyo.
Beki ya pembeni Mourinho atapata huduma nzuri kutoka
kwa Ashley Cole na Cesar Azpilicueta.
Wawili hawa wako fasta kwenye kushambulia na
watawapa Lampard na Modric wigo mpana zaidi wa kuanzisha mashambulizi kutoka
kati kati ya uwanja.
Lakini cha muhimu zaidi ni kuwa wawili hawa wanajua
kukaba.
Mwisho kabisa, kuna kipenzi kingine cha Mourinho,
kipa Cech, ushujaa wake umeipa taji Chelsea msimu uliopita na kumaliza kwenye
tatu bora katika ligi.
Kwa kiwango hicho na ujio wa Mourinho, mafanikio
yatakuwa mengi zaidi msimu ujao.
Thibaut Courtois kipa aliye kwa mkopo Atletico
Madrid, atarudishwa ilikumpa changamoto Cech katika goli la Chelsea.
Kwenye benchi Mourinho atatamani kumuona mchezaji
wake wa zamani alipokuwa Inter Milan, Wesley Sneijder akisubiri kuongeza nguvu
kwenye utatu mtakatifu.
Mourinho ameendelea kuwa karibu na staa huyo wa
Kiholanzi, ambaye hana amani Galatasaray tangu alipotua huko kwa ada ya pauni
milioni 7, Januari mwaka huu.
Demba Ba na Romelu Lukaku watakuwa wakisubiri.
Ramires anaweza kucheza kama beki wa kulia, kiungo wa kulia au kiungo wa ulinzi
wakati Luiz na Branislav Ivanovic watakuwa wakisubiri nje.
Mashabiki wa Chelsea wanasubiri kwa hamu kumuona
Mourinho kazini.
Jeshi
kamili la Mourinho
Kikosi
Kipa:
Petr Cech
Beki
wa kulia: Cesar Azpilicueta
Beki
wa kati: Raphael Varane
Beki
wa kati: John Terry
Beki
wa kushoto: Ashley Cole
Kiungo
wa ulinzi: Luka Modric
Kiungo
wa ulinzi: Frank Lampard
Kiungo
wa pembeni:Eden Hazard
Kiungo
wa pembeni:Oscar
Kiungo
mshambuliaji: Juan Mata
Mshambuliaji:
Edinson
Cavani
Mfumo:
4-2-3-1
Courtois
Ivanovic
Luiz
Ramires
Ba
Sneijder
Lukaku
No comments:
Post a Comment