Tena mimi... Neymar akishangilia baada ya timu yao ya Brazil kuifunga bao 4-2 dhidi ya Italy
Katika Mechi nyingine ya Kundi A, Mexico iliifunga Japan Bao 2-1 lakini Timu zote hizi mbili zilikuwa zimeshatolewa nje ya Masindano.
Huko Arena Fonte Nova, Mjini Salvador, Wenyeji Brazil waliongozwa na Staa Neymar ambae kwa mara nyine tena aling’ara na kufunga Bao safi la frikiki wakati Brazil walipoichapa Italy Bao 4-2.
Brazil walitangulia kufunga kwa Bao la Beki Dante lakini Italy wakasawazisha kwa Bao la Emanuele Giaccherini.
Emanuele Giaccherini akifunga bao dakika ya 55
Fred akiipatia bao la tatu Brazil
Referee Ravshan Irmatov kwenye patashika ya bao la Giorgio Chiellini
Wachezaji wa Brazil wakimzonga refa.
Fred akifunga bao la pili
David Luiz aliondolewa baada ya kuumia
Dani Alves akifanya mambo yake!
MAGOLI:
Brazil 4
-Dante Dakika ya 45
- Neymar 55
-Fred 66 & 88
Italy 2
-Giaccherini 51
- Chiellini 71
Brazil sasa watacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi B ambao leo Usiku wanamaliza Mechi zao za Kundi.
Brazil-Rekodi yao na Italy:
-Brazil hawajafungwa na Italy tangu Fainali ya Kombe la Dunia Mwaka 1982
-Brazil hawajafungwa Mechi ya Mashndano rasmi Nchini kwao Brazil kwa Miaka 40.
Katika Kundi B, Spain tayari wameshafuzu kucheza Nusu Fainali na Timu moja ambayo itaungana nayo ni kati ya Nigeria au Uruguay na Mechi zao za leo ndio zitaamua hilo wakati Spain watakapocheza na Nigeria na Uruguay kucheza na Tahiti.
***********************
MEXICO 2 vs JAPAN 1
BAO 2 za kichwa za Kipindi cha Pili za Straika wa Manchester United Javier Hernandez ‘Chicharito’ zimewafanya Mexico waondoke Brazil kwa ushindi baada ya kuifunga Japan Bao 2-1.
Nyavu...
Shinji wa United naye alikuwemo jana
Hernandez akikosa penati baada ya mkwaju wake kudakwa na kipa Eiji Kawashima
Japan wamemaliza Mashindano haya wakiwa mkiani mwa Kundi A bila kushinda hata Mechi moja na kufungwa Mechi zao zote 3.
No comments:
Post a Comment