Taifa Stars leo ikicheza ugenini imefungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kutafuta kufuzu kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Stars inayofundishwa na Kim Poulsen ilikutana na dhahama hiyo baada ya mchezaji wake Agrey Morris kutolewa nje kwa kadi nyekundu huku pia Morocco ikipata penalti dakika ya 37.
Mpaka mapumziko Morocco walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 na timunziliporudi uwanjani Morocco waliongeza bao lingine dakika ya 50 baada ya mshambuliaji wao kuwazidi mbio mabeki wa Taifa stars.
Taifa stars ikicheza pungufu ilipata bao la kufutia machozi toka kupitia kwa Amri Kiemba baada ya kuachia shuti la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Morocco.
Hiki ndicho kikosi kilichopo uwanjani leo Mrrocco.
Juma Kaseja (1) capt, Aggrey Morris (6), Patrick Kelvin Yondani (5),
Domayo Frank Raymond (16) Ngassa Mrisho Alfani (8), Erasto Nyoni (4), Salum
Salum Abubakar (2), Ulimwengu Thomas Emmanuel (11), Shomari Kapombe (20),
Mbwana Samattah (10), Ramadhani Amri (9).
Wachezaji wa Akiba ni
Mwadini Ali (18) Juma
Vicent (19), Ali Nurdin Haroub (13), Athumani Idd (3), Mwitula Mwinyi (15),
Abbas Mudathiri (17), Khamis Mcha (7), Msuva Simon (12), Chanongo Haruni (21),
BocoJohn (14), Shabani Pazzi Zahoro (22), Mtinge Ally Mustafa (23)
Wakati Taifa stars ikifungwa, wenzao Ivory coast imeshinda mabao 3-0 dhidi ya Gambia, mabao ya Ivory coast yamefungwa na Lasina Traure dakika ya 12, Wilferd Bony dakika ya 62 na Yaya Toure dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo Ivory coast inaongoza kundi ikiwa na pointi 10, Tanzania pointi 6, Morocco pointi 5 na Gambia wanabaki na ponti yao 1.
Kwa matokeo hayo Ivory coast inaongoza kundi ikiwa na pointi 10, Tanzania pointi 6, Morocco pointi 5 na Gambia wanabaki na ponti yao 1.
No comments:
Post a Comment