BRAZIL imetwaa Kombe la Mabara jana usiku baada ya kuifunga Hispania mabao 3-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro, Brazil.
Kwenye mchezo huo, mabingwa wa Dunia na Ulaya walipoteza mchezaji mmoja na pia wakashindwa kufunga kwa penalti.
Katika mchezo huo Fred aliyefunga mabao mawili, la kwanza dakika ya pili na la tatu dakika ya 47 kwa pasi iliyotoka kwa Hulk na Neymar aliyefunga la pili dakika ya 44 baada ya kupokea pasi iliyotoka kwa Oscar.
Pique alitolewa nje dakika ya 68 kwa kumchezea rafu, Neymar na dakika ya 54 Marcelo alimuangusha kwenye eneo la penalti Navas, lakini Sergio Ramos akakosa penalti kwani shuti lake lilitoka nje.
Kikosi cha Brazil kilikuwa: Julio Cesar; Dani Alves, Thiago Silva (capt), David Luiz, Marcelo; Oscar, Luiz Gustavo, Paulinho; Fred, Neymar, Hulk.
Hispania: Iker Casillas; Alvaro Arbeloa/Azpilicueta dk46, Gerard Pique, Sergio Ramos, Jordi Alba; Xavi, Sergio Busquets, Andres Iniesta; Juan Mata, Fernando Torres na Pedro.
Fred alifunga mabao mawili
Gerard Pique alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumuumiza Neymar
Sergio Ramos penalti yake iliota mbawa
Fred akishangilia bao lake la pili kwa timu yake Brazil ambalo pia ni la tatu
David Luiz aliokoa shuti la Pedro
Neymar akishangilia na mashabiki Maracana
Polisi wa kutuliza ghasia wakipuliza gesi ya moto kudhibiti fujo nje ya Uwanja wa Maracana
Fred akifunga
Fred alifunga dakika ya pili tu bao la kwanza
Fred akishangilia na Neymar
No comments:
Post a Comment