Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 6, 2013

BASSEY AMWAGA RADHI MJENGONI, WATANZANIA WATAKIWA KUMUOKOA FEZA KESSY

Bassey amwaga radhi mjengoni
SEBULE ya jumba la Ruby juzi iligeuka ukumbi wa muziki, baada ya washiriki kukusanyika eneo hilo na kuanza kucheza muziki, huku kila mtu akitoa staili zake ilimradi abambe tu.
Ilionekana kama pombe walizokunywa mapema siku iyo ndizo ziliwatuma kucheza muziki siku hiyo, baada ya muziki kunoga ilikuwa zamu ya Bassey wa Sierra Leone na Beverly wa Nigeria kuonyesha utaalamu wao.
Bassey alianza kucheza muziki na kisha kuvua nguo zake zote na kubaki na ‘boxer’ nyeupa kisha kuanza kuyarudi huku akiwapandia baadhi ya wasichana wa Jumba hilo.

Pombe ndiyo kila kitu BBA
CHAKULA kinaweza kuwa ndiyo kitu pekee kinachopendwa na kila mtu ulimwenguni, lakini kwa washiriki wa Big Brother waliondani ya jumba la Ruby, pombe ndiyo kila kitu kwao.
Kasi ambayo washiriki hao walikuwanayo walipoambiwa na Biggie kuwa stoo iko wazi wanaweza kuchukua mahitaji yao, wanaweza kumpita hata Usain Bolt, lakini cha ajabu walipoingia stoo hakuna aliyeshughulika na chakula wote walikimbilia chupa za mitungi.
Na walipopata pombe hizo walianza kucheza kwa furaha, huku LK4 na Natasha wakichukuana na kucheza kwa pamoja, Koketso naye alikuwa pembeni yao akifurahi tu, Sulu yeye alitumia nafasi hiyo kujisogeza kwa Selly na kucheza kwa karibu sana.

Watanzania watakiwa kumuokoa Feza Kessy
WATANZANIA wametakiwa kumpigia kura Mtanzania, Feza Kessy ili aendelee kubaki kwenye shindano la Big Brother Africa The Chase, baada ya Mbongo huyo kupigiwa kura ya kuingia kikaangoni wiki hii.
Watanzania wanaweza kumpigia kura Feza kubaki BBA kupitia mtandao, kwa njia ya simu na kwa njia ya meseji.
Kwa upande wa mtandao unaweza kumuokoa Feza kwa kuingia kwenye www.bigbrotherafrica.dstv.com na kupiga kura mara moja kila baada ya saa moja, pia unaweza kupiga kura hadi 100 kwa njia ya meseji.
Jinsi ya kupiga kura kwa Meseji unaandika jina la Feza kwenda kwenye namba 15456, kupitia mitandao ya Vodacom, Tigo, Zantel na Airtel na kila meseji ni shilingi 600 tu.
Wengine walioko kikaangoni ni pamoja na LK4, Dillish, Hakeem na Koketso.



No comments:

Post a Comment