PARIS, Ufaransa
MCHEZA tenisi, Jo-Wilfried Tsonga, amemtupa nje ya michuano ya wazi ya Ufaransa,
nyota anayeshika nafasi ya pili kwa ubora, Roger Federer na hivyo kurejesha
matumaini kwa nchi yake kutwaa ubingwa wa dunia upande wa wanaume baada ya
miaka 30 ya ukame.
Kwa ushindi huo wa juzi, jana Tsonga alitarajia kumkabili David Ferrer katika hatua ya nusu fainali.
“Nadhani nilipata ushindani mdogo kiasi kila mahali. Nina masikitiko kidogo kuhusu mechi hii na kwa jinsi nilivyocheza,” alisema Tsonga, mara baada ya mtanange huo.
Serena atinga nusu fainali kwa tabu
MCHEZA tenisi ambaye anashika nafasi ya kwanza kwa ubora
ulimwenguni, Serena Williams, amenusurika kichapo kutoka kwa bingwa wa
zamani, Svetlana Kuznetsova, baada ya kushinda kwa tabu mechi yake ya robo
fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa.
Bingwa huyo wa michuano hiyo ya Roland Garros ya mwaka 2002, ndiye aliyeshinda seti yake ya kwanza kwa urahisi kabla ya kupoteza zote na kumfanya raia huyo wa Russia kufungwa seti 6-1 3-6 6-3.
"Mechi ilikuwa ni ngumu na nilikuwa nimechoka," alisema Serena, ambaye ni mwanamke wa kwanza raia wa Marekani kutinga hatua ya nusu fainali tangu mwaka 2004, wakati Jennifer Capriati alipotinga hatua hiyo.
Katika mechi nyingine, David Ferrer kutoka Hispania alimuadhibu Mhispania mwenzake, Tommy Robredo kwa seti 6-2 6-1 6-1 na hivyo kukata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali kwa mara ya pili mfululizo.
Laura Robson kunolewa na mwalimu wa zamani wa Murray
NYOTA wa mchezo wa tenisi, Laura Robson, ataanza kujifua
chini ya kocha wa zamani wa Andy Murray, Miles Maclagan, ili aweze kujiandaa
kufanya vyema katika mashindano
mbalimbali.
Kwa mujibu wa
vyanzo vya habari, nyota huyo alitarajia kuanza kibarua hicho jana, huku akiwa
na mtazamo wa kumpa mkataba wa kudumu.
"Tutaanza kufanya kazi pamoja kwa muda ili tuone jinsi hali itakavyokuwa," Maclagan aliiambia BBC Radio 5.
Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza mwenye umri wa miaka 38, alimfundisha Murray kuanzia mwaka 2007 hadi 2010, na tangu kipindi hicho alikuwa akifanya kazi na Mjerumani, Philipp Kohlschreiber na Cypriot Marcos Baghdatis.
Alipohojiwa atakavyofanya kazi katika ziara za wanawake ikiwa ni mara ya kwanza, Maclagan alisema: "Hii itakuwa changamoto mpya na ndiyo maana tunaanza kwa kufanya kazi kwa majaribio ili tuweze kuona kitakachojitokeza,” alisema kocha huyo.
No comments:
Post a Comment