Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 22, 2013

STARS YAJAZWA MANOTI KUSAIDIA KUIUWA MOROCCO

Wajumbe wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde, wakiwakabidhi nahodha wa Stars, Juma Kaseja na Meneja Leopold Taso Mukebezi, (kushoto), kitita cha sh milioni 30 kama moja ya hamasa kwa timu hiyo kufanya vema katika kinyang’anyiro cha kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil. Kutoka kulia ni Dk. Ramadhani Dau, Zitto Kabwe, Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye ndiye Mwenyekiti, Leodegar Tenga na Teddy Mapunda. 


WACHEZAJI wa timu ya Taifa,  Taifa Stars jana walikabidhiwa Milioni 30, ikiwa ni pongezi ya kufanya vizuri dhidi ya Zambia na Morocco, huku wakiwatakiwa kuhakikisha wanashinda mechi ya marudiano dhidi ya Morocco.
Akizungumza jijini juzi, wakati wa kukabizi fedha hizo kwa wachezaji, Mwenyekiti wa Kamati ya ushindi ya Taifa Stars, Mohammed Dewji alisema timu hiyo inastahili pongezi kwa juhudi iliyoweza kuonyesha.
Dewji alisema wachezaji wameweza kurudisha heshima ya Tanzania, huku  akiwataka wahakikishe wanaonyesha nidhamu ya hali ya juu ili wafanikiwe zaidi.
“Nidhamu itasaidia timu yetu kufika mbali zaidi ya hapa, kila mchezaji anatakiwa kuwa na jukumu kujituma zaidi ya mwingine ili tutaweze kufikia malengo yetu,” alisema
Alisema ni vizuri kila mchezaji wa timu hiyo, akawaza mpira zaidi ya kitu kingine, ili kujiongezea uwezo wa kufikiri na mbinu mbalimbali za kusaidia timu yake.
“Inatakiwa kuanzia sasa, wachezaji wote wawaze mpira, vizuri ukilala na kuamka ukawaza jinsi gani utaweza kuisaidia nchi yako na kuifanyia makubwa kupitia soka,”alisema
Mwenyekiti huyo alisema mbali na fedha hizo waliozotoa, Kamati hiyo itaendelea kusaidia timu hiyo ili iweze kufanikiwa, huku kila kiongozi akiwa amepewa majukumu yake.
Katika hatua nyingine, kocha wa timu hiyo Kim Poulsen alisema anaimani kikosi chake alichokichagua  kitafanya vizuri, kwani ameshaona mwangaza huo katika mechi mbalimbali walizocheza.
Timu hiyo ipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea Morocco katika mchezo wake wa marudiano utakaofanyika Julai mwaka huu, huku ikitarajiwa kujipima nguvu dhidi ya Sudan  nchi Ethiopia  kabla ya kuvaana na Morocco. 
Taifa Stars, iliweza kuibuka na ushindi hapa nyumbani kwa kuifunga Morocco bao 3-1, mechi hiyo ikiwa ni kuwania kufudhu kucheza kombe la  dunia mwakani .

No comments:

Post a Comment