Neymar
MARA kwa mara kinda kutoka Brazil,
huibuka akiwa amejaliwa kipaji cha hali ya juu na kuanza kulinganishwa na Pele.
Huyu ni mhitimu kutoka chuo cha soka cha Santos, amekuwa akitajwa mmoja kati ya
wachezaji makinda wanaotarajiwa kuja kufanya makubwa sana ulimwenguni, aina
yake ya uchezaji inafananishwa na Garrincha na ile ya Romario, japo bado yuko
nchini kwao Brazil jina lake ni kubwa zaidi duniani kwa sasa.
THOMAS
MULLER
UKUAJI wa kasi wa Thomas Muller kwa kiasi kikubwa anatakiwa
kumshukuru kocha wa zamani wa Bayern Munich, Louis van Gaal, mtu ambaye alikuwa
tayari kumuamini na kumpa mechi yake ya kwanza katika klabu hiyo msimu wa
2009-10, tangu hapo amekuwa moto wa kuotea mbali na ubora wake umethibitika
wiki iliyopita kwa mabao yake mawili dhidi ya Barcelona.
UBORA WAO
Neymar: Ni mchawi akiwa na mpira mguuni kwake, kasi yake, uwezo wa
kukokota mpira, umaliziaji mzuri na mbinu zake za hali ya juu zinamfanya awe
mtu hatari kukutana naye. Ufahamu wake mkubwa wa soka na akili ya ziada
uwanjani, vinamfanya aweze kucheza kama winga au mshambuliaji wa kati.
Muller: Anajua
kwa nini ni mchezaji wa kulipwa na tabia yake ya upole, imemfanya awe na
marafiki wengi, uwezo wake wa kuona mbali, ufundi na utulivu akiwa na mpira
vinamfanya awe tofauti kabisa na wachezaji wengi.
UDHAIFU WAO
Naymer: Nidhamu yake inaanza kuzua maswali, kutokana na kuhusika
kwenye matukio kadhaa ya kinidhamu, pia watu wamekuwa wakimlaumu kwa tabia yake
ya uchoyo anapokuwa na mpira, pamoja na matumizi ya mchezo mbaya kwenye soka.
Muller: Bado
anahitaji kukomaa zaidi na kuongeza ukakamavu zaidi kwa sababu kuna wakati
hutoka nje ya mchezo.
KIPINDI
KIZURI
Naymer: Mabao yake mawili dhidi ya Scotland,
Machi 2011 ilifikisha idadi ya mabao yake kwenye timu ya taifa kufikia matatu
kwenye mechi tatu na kutambulisha kipaji chake zaidi ulimwenguni.
Muller: Kushinda
tuzo ya mchezaji bora kijana kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2010, pia
alishinda tuzo ya ufungaji bora wa michuano hiyo akiwa na mabao matano na
kutengeneza mengine matatu.
KIPINDI KIGUMU
Naymer: Septemba 2010, Neymar alionyesha upande wake wa pili baada
ya kuzua mzozo kwenye mechi dhidi ya Ceara, na baadaye kugombana na kocha
Dorival Junior, baada ya kukatazwa kupiga penalti dhidi ya Guarani. Dorival
alimuadhibu hilo liliukera uongozi na wakamtimua kocha huyo.
Muller: Msimu wa
2008-09 aliingia mara nne akitokea benchi, lakini alishindwa kujitengenezea
namba.
STAILI YA UCHEZAJI
Naymer: Anasisimua, mbunifu, mgumu kumzuia na ni mshambuliaji
hatari sana.
Muller: Anakasi,
hatari, mpigaji mzuri wa pasi na anaona mbali.
KAULI
Neymar: “Ni vizuri
kulinganishwa na mchezaji bora (Pele). Lakini baba yangu aliniambia kuhusu soka
la Garrincha wakati akiwa anashambulia, anakokota mipira. Staili ya Garrincha
inalingana na ya Neymar,” alisema Neymar,
Januari 2011.
Muller: “Miezi
12 iliyopita nilikuwa nawaza kama naweza kuchezea Bayern kwenye Bundesliga.
Lakini sasa hivi niko kwenye timu ya taifa
ni kama ndoto. Haiwezi kuwa bora zaidi ya hapa,” alisema Muller.
USICHOKIJUA
Neymar: Zaidi ya mashabiki
14,000 wa Brazil walitia saini karatasi ambayo ilikuwa ikimlazimisha Dunga
kumuita Naymer kwenye kikosi kilichoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini
Afrika Kusini.
Muller: Wakati
wa Kombe la Dunia 2010, Diego Maradona alikataa kukaa kwenye mkutano na
waandishi wa habari akiwa na Muller kwa sababu hakujua alikuwa mwanasoka.
Lakini baada ya Ujerumani kuipiga Argentina 4-0, Muller alisema: “Linapokuja
suala la Maradona, hii ni nzuri kwangu. Sidhani kama ataendelea kudhani kuwa
mimi ni muokota mipira.
WASIFU
Neymar
- Jina Kamili: Neymar da Silva Santos Junior
- Namba ya jezi: 11
- Umri: Miaka 21
- Kuzaliwa: Februari 5, 1992
- Alikozaliwa: Mogi das Cruzes, Sao Paulo, Brazil
- Urefu: futi 5 na inchi 9
- Uzito: Kilo 60
- Klabu: Santos
- Taifa: Brazil
Thomas Muller
·
Namba ya Jezi: 25
·
Nafasi: Kiungo/Mshambuliaji
·
Umri: Miaka 23
·
Kuzaliwa: Septemba 13, 1989
·
Alikozaliwa: Weilheim, Ujerumani
·
Urefu: Futi 6.2
·
Uzito: Kilo 74
·
Klabu: Bayern Munich
·
Taifa: Ujerumani
No comments:
Post a Comment