Viongozi wa benki za DCI, NIC, CRDB, BancABC na MGen Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kutia saini makubaliano |
Viongozi wa mabenki na shirika la Nyumba wakiwa kwenye picha ya pamoja |
Wadau wakifuatilia kwa makini jinsi mambo yanavyokwenda |
BENKI nne za
jijini Dar es Salaam, zimesaini makubaliano na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
kwa ajili ya kuwakopesha wananchi fedha za kununulia nyumba zinazojengwa na
shirika hilo.
Makubaliano hayo
yalisainiwa jijini Dar es Salaam leo kati ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NHC,
Felix Maagi na viongozi wakuu wa benki hizo.
Benki
zilizosaini makubaliano hayo ni DCB, ABC, NIC pamoja na Benki ya CRDB.
Akizungumza
wakati wa makubaliano hayo, Maagi alisema yamefanyika kama sehemu ya mwendelezo
wa taasisi za fedha kushirikiana na NHC kuwafanya wananchi wamiliki nyumba.
“Kama
mtakumbuka, mwaka juzi tulisaini makubaliano na mabenki manane kwa ajili ya
kuwasaidia wananchi kuweza kumiliki nyumba.
“Kwa faida ya
wale ambao hawakuwapo wakati tunasaini makubaliano ya kwanza, ni kwamba
tulisaini na Benki za Azania, BOA, CBA, Exim, KCB, NBC, NMB na Benki ya
Stanbic.
“Kwa maana
hiyo, kitendo cha kusaini makubaliano na mabenki haya manne leo ni mwendelezo
wa utaratibu wetu wa kushirikiana na taasisi za fedha katika kuwakomboa
wananchi, hasa hasa katika umiliki wa nyumba,” alisema Maagi.
Kwa mujibu
wa Maagi, lengo la shirika hilo ni kuwafanya wananchi waachane na tabia ya
upangaji, badala yake wawe na uwezo wa kumiliki nyumba zinazojengwa na kuuzwa
na shirika hilo kupitia mikopo inayotolewa na benki mbalimbali.
Naye
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima ya MGen Tanzania, Charles Sumbwe, ambaye kampuni
yake imesaini mkataba na NHC kwa ajili ya kuwadhamini wananchi wa kipato cha
chini ili nao waweze kumiliki nyumba, alisema kampuni yake imelazimika kusaini
mkataba huo, baada ya kuguswa na tatizo la wananchi wengi kutokuwa na uwezo wa
kumiliki nyumba.
“Moja ya
majukumu ya kampuni yetu ni kuwasaidia wananchi, kwa hiyo, tumeamua kujitosa
katika kuwadhamini wananchi wenye uwezo mdogo kifedha ili nao waweze kumiliki
nyumba kama ilivyo kwa wenye nazo,” alisema Sumbwe
No comments:
Post a Comment