Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 13, 2013

ROONEY ANAHISI MAN UNITED WANAMSALITI NA KUMFUKUZA KIJANJA




MANCHESTER, England
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney (27) anajiona kama amewekwa kwenye wakati mgumu na kusalitiwa, baada ya mazungumzo yake binafsi na Sir Alex Ferguson kuvuja.
Alipoingia ofisini kwa Ferguson, wiki tatu zilizopita, Rooney alihitaji majibu ya kwanini anaonekana kama siyo sehemu muhimu ya Man United.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu na Kambi ya Rooney, anasema Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa muhimu Old Trafford, tangu alipotua mwaka 2004, alikuwa amepania kumuuliza Fergie kwa nini anaonekana amepoteza imani naye.
Rooney alihitaji kujua ana nafasi gani ndani ya kikosi cha Ferguson siku zijazo, na alimwambia wazi Fergie kuwa hataki kuwa na msimu mwingine mgumu kama huu akihamishwahamishwa kikosini.

Lakini baada ya kumaliza kikao chake na Fergie dakika 25 baadaye, Rooney alikuwa hana uhakika na mustakabali wake Old Trafford, kutokana na Ferguson kutomuahidi lolote, juu ya nafasi yake kwenye timu.
Cha ajabu kila kitu kilichotokea kwenye mazungumzo yake na Fergie kilivuja, kitu ambacho kimemfanya Rooney ajione kama anatafutiwa sababu ya kuondolewa Man United, huku Red Devils wakipiga hatua ya kwanza katika kile kinachoonekana kama mwisho wake.

Mtu huyo wa karibu na Rooney anasema wazi anaamini kuwa, majadiliano yake na Fergie hayakutakiwa kutangazwa hadharani, japokuwa hataki kuamini kuwa Ferguson ndiye aliyevujisha siri hiyo.
Rooney anajiona kama amesalitiwa kutokana na kuvuja kwa habari hizo, huku akishitushwa na taarifa kwamba aliweka mezani madai ya kuondoka Old Trafford, kitu ambacho anakikanusha kwa nguvu zote.
Man United, wamekanusha taarifa kuwa Rooney aliomba kuondoka, tayari klabu hiyo imesema kwamba, haina mpango wa kumuuza.

Inasemekana Rooney na Ferguson, walikubaliana kulijadili jambo hilo kwa kina baada ya mechi dhidi West Brom, Jumapili ijayo. Lakini Sasa hivi Rooney haelewi nini kitamkuta baada ya Fergie kustaafu.
Sakata hilo ndio kitu cha kwanza kitakachotua kwenye meza ya David Moyes, Julai 1, atakapoanza kazi rasmi, labda kama Man United wakiamua kumuuza kabla ya hapo.

Gwiji wa Man United, Bryan Robson amemshauri David Moyes kumshawishi Rooney kubaki Old Trafford, kwa sababu kufanya hivyo itakuwa hatua ya kwanza muhimu kwake katika kujitengenezea jina miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment