Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 13, 2013

LIREFA YALAANI VURUGU ZILIZOTOKEA WAKATI WA MCHEZO WA LIGI YA MABINGWA JUZI



UONGOZI wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Lindi (LIREFA), umelaani vikali vurugu zilizotokea kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani humo, wakati wa pambano la Kariakoo dhidi ya Titanic ya Nachingwea ya Mtwara.

Akizungumza na BINGWA jana Katibu Mkuu wa LIREFA, Luis Taisamo,  alisema pambano la timu hizo lilivunjika katika dakika ya 67, kutokana na vurugu kubwa zilizosababishwa na mashabiki wa soka.

Alisema vurugu hizo zinadaiwa kufanywa na baadhi wa mashabiki wa Titanic, Chama chake kinalaani kitendo hicho kwa nguvu zote, kwa maelezo kuwa hakiendani na maadili mema ya mchezo wa soka.

Alisema kuwa LIREFA kimesikitishwa na kitendo hicho, kimeona ni vyema kitoe tamko la kulaani wale wote waliohusika na vurugu hizo, ambazo zilisababisha usumbufu kwa mashabiki wengine wasio na hatia. 

“LIREFA tunalaani vurugu zilizotokea kwenye uwanja wa Ilulu, ambazo zilisababisha mechi ya fainali uwanjani hapo kuvunjika, pia na kusababisha usumbufu kwa wengine waliofika kushuhudia pambano,” alisema Taisamo.

Akifafanua alisema, kamati yake ya Utendaji imeipa Kariakoo ubingwa wa Mkoa wa Lindi, wakati pambano lilipovunjika ilikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Nassoro Cholo na Salum Abdil.

No comments:

Post a Comment