Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 9, 2013

INAFANANAJE KUMZUIA MESSI



LIONEL Messi alifunga mabao 91, mwaka 2012, hii inamaanisha kwamba kuna wakati kwenye mwaka huo, mabeki 91 walifanywa waonekane wapuuzi katika kazi yao.
Ndio inajulikana kwamba idadi ya mabeki waliofanywa wapuuzi ni kubwa kuliko hiyo. Messi anapoingia uwanjani, wachezaji wenzake kwenye timu yake wanapata ari, wakati mabeki hata kama ni bora duniani wanapata kitete.

Messi ni mfupi, lakini kwenye soka ni bonge la mtu. Akiwa na miaka 25 tu, tayari anatajwa kama mmoja kati ya wachezaji bora wa kizazi chake na mmoja kati ya bora wa muda wote.
Inafananaje kukabana na Messi? Hapa inaangaliwa kiufundi zaidi. Lakini hakuna beki ambaye anaweza kudiriki kusema kwamba kumkaba Messi ni rahisi, kuna baadhi wamefanikiwa. Katika kujaribu kutafuta jibu la hili swali, makala haya yameangalia wakati bora na mbovu kwenye maisha ya soka ya Messi.

Kiufundi zaidi
Messi alikuwa kabla ya kutengenezwa na kuwa mashine ya ufungaji chini ya usimamizi wa Pep Guardiola, Barcelona. Akicheza kama namba tisa wa uongo (False 9), Messi anacheza chini zaidi tofauti na namba tisa wa kawaida anavyotakiwa kucheza, hii inawapa wakati mgumu sana mabeki wa timu pinzani kumkaba ‘Man to man’.

Chini ya Guardiola Messi alicheza kati na David Villa kushoto. Villa alikuwa akiingia kati kati na Messi kukimbilia pembeni, ili kuwachanganya mabeki. Tito Vilanova aliiga mfumo huu wakati wa mechi ya pili ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan na matokeo yalikuwa mazuri kwa Barca.

Barcelona inacheza kumzunguka au kwa kumuangalia Messi, ambaye ana majukumu madogo sana ya kukaba, ili kumfanya asichoke. Licha ya mfumo pia uwezo binafsi wa Messi kwenye kumiliki mpira, kasi, kuchanganya haraka akiwa anakimbia, kuusoma mchezo, kasi ya miguu yake na uwezo mkubwa wa kubadili mwelekeo.
Kumalizia ni kwamba, Messi anajua kuutumia mguu wake wa kushoto hivi vyote vinamfanya yeye na Barca kutisha ulimwenguni.

Kutafsiri mbinu uwanjani
Wakati Chelsea wakijiandaa kukutana na Messi pamoja na Barcelona kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa 2011-12, Kocha wa muda wa The Blues na timu yake Roberto Di Matteo, walihangaika sana kutafuta mbinu sahihi za kuzuia soka la pasi la Barca. Huku Messi akijadiliwa zaidi.

“Uwezo wake akiwa na mpira ni balaa, lakini cha muhimu zaidi anaweza kubadilika kadri mechi inavyosonga mbele,” kipa wa Chelsea, Petr Cech alinukuliwa na gazeti la Daily Telegraph. “Dakika za mwisho katika mazingira yoyote anaweza kupata suluhisho la tatizo lolote, kuna staili nyingi anaweza kutumia kumalizia mashambulizi.”
Cech aliongeza: “Kwa upande mwingine, ni mtu wa kawaida kama wengine, kama tukicheza kwa asilimia 100, tutaweza kujilinda dhidi yake.”

Maneno ya mwisho ya Cech yalikuwa sahihi. Chelsea walimkera Messi na kuifunga Barcelona kwenye nusu fainali kwenye msimu huo, kabla ya kusonga mbele na kuchukua ubingwa wakitumia mfumo wa ‘kupaki basi’. Japokuwa unaweza kusema kuwa bahati ilikuwa yao kwenye msimu huo.
Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora msimu huu, AC Milan walishinda 2-0 kwenye mechi ya kwanza, San Siro, walicheza soka la kujilinda zaidi kama Chelsea msimu uliopita. Ushindi huo haukuwasaidia, kwa sababu kwenye mechi ya marudiano Barca, ikiwa na Messi aliyekuwa kwenye fomu, iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, matokeo ambayo yalimuacha kocha wa Milan, Massimiliano Allegri akiumwagia sifa ‘Utatu mtakatifu’ wa Barca, Messi, Xavi Hernandez na Andres Iniesta.

Hapo pia kuna sababu nyingine ambayo inaongeza ugumu kwenye kumzuia Messi. Timu inawezaje kumzuia Messi na mfumo mzima wa Barca wa pasi na umiliki wa mpira?
“Ukimuona Iniesta anavyokokota mpira kwa dakika 90 bila kuchoka, unaweza kugundua vitu vingi sana,” Allegri alinukuliwa na gazeti la The Independent. “Ni moja ya timu ngumu zaidi duniani na wana wachezaji watatu wa kipekee Messi, Xavi na Iniesta."

Zaidi ya mbinu
Messi ana mchango mkubwa Barca ambao hata mtaalamu wa kawaida hawezi kuuelezea. Kwenye msimu huu wa ligi ya mabingwa, Messi alipata majeruhi kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali dhidi ya Paris Saint-Germain. Kwenye pambano la Nou Camp alianzia benchi, aliingia uwanjani kipindi cha pili wakati timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0.

Mara baada ya kuingia uwanjani, mechi ikabadilika. Uwepo wa Messi ulionekana kuongeza ari kwa wachezaji wengine wa Barcelona. Barca walipata bao dakika chache tu, baada ya Messi kuingia wakapata sare ya 1-1 wakaenda nusu fainali.
Wote Barca na PSG walibadilika baada ya Messi kuingia uwanjani, hii ni kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la England.

Baada ya filimbi ya mwisho Villa alisema: “Messi ni mchezaji bora wa dunia, na alibadilisha kila kitu kwa uwepo wake uwanjani.” Alinukuliwa Villa na gazeti la Daily Telegraph. Wakati kocha wa PSG Carlo Ancelotti yeye alisema: “Ni wazi Messi aliwaongezea kujiamini timu yake, kwa sababu hata kama hayuko fiti asilimia 100 bado ni mchezaji wa kipekee.”
Katika hili, mbinu na kipaji havikuwa muhimu. Uwepo wa Messi uwanjani ulitosha kuifufua timu yake na katika hilo hakuna kocha wa timu pinzani ambaye ameweza kujua mbinu ya kuzuia hilo.

Inavutia
Kwenye timu ya taifa ya Argentina, Messi amefunga mabao 32 kwenye mechi 79. Rekodi yake ya kufunga huku haiendani na rekodi yake akiwa na Barcelona, lakini hilo linaweza kutetewa na ukweli kuhusu soka la kimataifa.
Tofauti na Barcelona, wachezaji ambao wanatengeneza timu ya taifa ya Argentina wanakutana mara chache sana. Hawajazoea kucheza pamoja kama ilivyo kwa Xavi na Andres Iniesta. Pia wakati Messi akiangalia zaidi ushambuliaji wa Argentina, lakini timu hajajengwa kumtegemea yeye.

ya kumlinda iwe rahisi, Argentina walicheza na Marekani Machi 2011, ilikuwa mechi ya kirafiki ilichezwa katika Jiji la New Jersey.
Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 1-1, siku hiyo Messi hakufunga bao, kipa wa Marekani, Tim Howard, anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Everton, aliita kujipanga kwa Messi uwanjani kama kunavutia sana kumuangalia.

Kuna makala moja, iliandikwa kuelezea staili ya soka ya Argentina kwa wakati huo, staili ambayo inahusisha upigaji wa pasi fupi fupi za haraka na kumtengenezea mpira wa mwisho Messi kutokea katikati. Lakini kama Messi hakuhusika kwenye kumalizia shambulizi hilo, basi alikuwa kati ya uwanja akihusika kwenye kuanzisha mashambulizi, kama ilivyo akiwa Barcelona.
Kuelezea hilo, Howard alisema Messi huonekana kama anayetaka kupiga pasi siyo shuti: “Siku zote huwa najaribu kusoma miguu yake, na kuona wapi pasi inaenda na kusoma wachezaji wengine wanaoweza kuleta madhara kutokana na pasi zake.”

‘Mchawi’
Kwa kumalizia, kitu muhimu zaidi katika kumzuia Messi kwa mujibu wa Howard, ni kutokuwa na papara wala kupaniki mkimuona, Messi anaweza ‘uchawi’ wake na kufunga kabla hata mabeki kujua nini kimetokea.

Lakini cha kutisha zaidi kwa mabeki ni kwamba Messi huwa hasubiri mpaka mtu akosee ndio afunge. Kama ambavyo kiwango chake cha mwaka 2012 kilivyothibitisha kwamba mchawi huyo anaweza kuizuru beki ya timu yoyote muda wowote.
Hata pale timu yake inapofungwa Messi hufanya jambo ambalo huwaacha watu vinywa wazi.

Beki wa Chelsea, John Terry aliwahi kusema: “Kwangu mimi Messi ni mchezaji bora wa muda wote, ni mtu poa sana, na ni heshima kwa mchezaji kwangu mimi anakila kitu. Ni Mchawi.”

No comments:

Post a Comment