Mpendwa Gotze. Jan Aage Fjortoft alipotuma ujumbe wake kwenye Twitter usiku wa Aprili 22 akidai kwamba gazeti la Bild litatoka na habari kubwa ya usajili kwa usiku huo, sikuweza kupata ufahamu mapema ni habari gani hiyo. Niliipuuza.
Dakika chache baadaye, ikaibuliwa habari yenyewe iliyoshitua wengi: "Mario Gotze anakwenda Bayern."
Sikuwa mwenye kuamini na niliona kama ni uzushi. Niliamini kwamba utakuwa ni uzushi tu, lakini baadaye sote tukafahamu ukweli. Asubuhi yake, Dortmund walithibitisha jambo hilo.
Mwanzoni, nilikuwa siamini na niliona kama usaliti mkubwa. Na kujiuliza, ni wewe, kipenzi changu Mario, unakwenda kujiunga na maadui zetu wakuu, hilo liliniumiza sana. Niliamini tangu aliposhangilia bao akiwa na jezi ya Dede, niliamini mchezaji huyo angebaki kwenye klabu yetu daima.
Lakini, kwa upande mwingine nilikubaliana na hali halisi na sikuona kama ni kitu kinachoshangaza. Siku zote nilikuwa na ufahamu kwamba alikuwa akihitaji mambo makubwa, mambo ambayo yanaweza kukufanya ukasahau hata mapenzi ya dhati na utu.
Mashabiki wengi wa Dortmund wanauchukua uamuzi wako kama usaliti, lakini jambo hilo lipo wazi, ni suala la ndoto tu. Bayern imefika fainali tatu za Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya nne za hivi karibuni na wana mipango ya kuwa timu bora zaidi Ulaya miaka michache ijayo.
Vitu kama hivyo na kufanya kazi na makocha wenye viwango vya dunia kama Pep Guardiola, ni jambo linaloweka bayana kwa nini hukushawishika kuhamia ng'ambo na ukaamua kwenda Allianz Arena.
Nina hakika pia alishawishika na mshahara wa euro milioni 10 kwa mwaka, kitu ambacho isingekuwa rahisi kukipata kama ungebaki kwenye timu yetu.
Hivyo basi, kwa kutazama ukweli wa mambo ulivyo, hakuna sababu ya maelfu ya mashabiki wa BVB kuvunjika moyo kutokana na kuondoka kwako. Lakini, kwa bahati mbaya si kitu rahisi.
Soka ni mchezo unaotawaliwa na hisia - kuliko mchezo mwingine wowote na watu wamekuwa na hisia zenye nguvu ya ajabu kuhusu klabu zao. Timu hii ya Dortmund inanikosha kwa kucheza soka la burudani kubwa. Walivyo wachezaji wake ni kama kundi la marafiki wanaocheza bila kujali kitu, fedha na umaarufu vinakuja baadaye.
Watu wanaweza kuwaonyesha vidole Shinji Kagawa na Nuri Sahin, lakini wawili hao waliondoka Signal Iduna Park kwenda kutimiza ndoto zao, lakini huyo Gotze kuondoka kwake kumekuwa na sababu tofauti.
Uamuzi wako unahisiwa tofauti kwa sababu umeibukia kwenye akademi ya Dortmund. Kama anavyosema mchezaji mwenzako, Mats Hummels kwamba wachezaji wa Ujerumani wamepanga kuisaidia BVB kuwa kwenye daraja la juu.
Mataji na medali si kitu muhimu kwa Hummels tangu alipoanza kufikiria zaidi mambo mengine muhimu. Daima nguvu ya timu kama Bayern hakikuwa kitu kinachoweza kumshawishi.
Hii ilikuwa tofauti na wewe, siwezi kukuwekea tena mdhamana, hasa ukizingatia kwamba kila mtu anakuchukulia tofauti. Utoto wako ukichanganya na ushawishi wa wakala na chimbuko lake kuwa ni Bavaria hilo limekuwa sababu muhimu ya kuondoka.
Siwezi kukataa namna ulivyonihuzunisha. Misimu mitatu iliyopita Dortmund ilionyesha uhakika wa kuwa na timu bora kabisa, lakini kuondoka kwa mchezaji tuliyemtengeneza wenyewe hilo ni jambo linaloumiza.
Hii haina tofauti na kama vile kuamka kwenye njozi tamu. Kitu kinachoniumiza mimi ni kuona unakosa sifa kwa mashabiki wa timu yako mpya.
Umeona wazi kuhama nchi ya ng'ambo ingekuwa ngumu kupata sifa zinazostahili, lakini kitendo chake hicho kimekuponza na kukosa sifa unazostahiki. Baada ya mechi mbili za nyumbani msimu huu, nadhani ni Patrick Owomoyela, ndiye aliyekuwa mkono wa kwa heri, wengine wamebaki na hali yao ya hasira kwa sasa.
Ulijifanya kuipenda Dortmund sana, lakini klabu ilikuamini na kukuvisha deni kubwa la uaminifu.
Kilichobaki kwangu ni kusema asante tu kwa miaka yote uliyokuwa hapa. Ilikuwa furaha kukutazama ukicheza kwenye uwanja safi kabisa wa soka hapa duniani. Ulikuwa mtu wa kipekee katika nyakati zangu kama shabiki wa timu.
Utakapovaa jezi za Bayern msimu ujao, itakuwa kosa kubwa na kwamba nitachukulia hasira kama utaendelea kufanya vyema kwenye Bundesliga.
Binafsi sitaungana na mashabiki wengine, sitaimba nyimbo wala kupiga miluzi ya kukuzomea wakati utakaporejea kucheza Dortmund ukiwa na kikosi chako cha Bayern.
Nafahamu kwamba umefanya uamuzi unaoeleweka, hasa kwa umri kama wa kwako, ambao ulichangiwa na uzoefu finyu wa mambo ya maisha. Nilidhani kwamba ungekuwa fiti kucheza mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern kwenye Uwanja wa Wembley jana, ili tukushangilie kwa mara ya mwisho. Tulitaka kuona kile ambacho ungeweza kuifanyia BVB katika siku yako ya mwisho. Nakutakia furaha tele wewe na familia yako jijini Munich.
No comments:
Post a Comment