Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 4, 2013

YANGA NOMA, YAANIKA WAZI MCHORO WA UWANJA WAO UTAKAOCHUKUA WATU 40,000

KAMPUNI ya Beijing Construction Engineering Group, imeonyesha rasmi picha za Uwanja Mpya wa Yanga utakavyokuwa mara baada ya kuingia mkataba wa ujenzi wake mwishoni mwa mwezi ujao kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.

“Utakuwa ni uwanja wenye hadhi na uwezo mzuri kiasi ambacho kitaiweka Yanga katika kiwango kizuri mno, ingawa hayo pia yatategemea makubaliano yetu na klabu kwa ujumla.

Katika ujenzi huu kwanza tulipewa kazi ya kuandaa ramani nzuri kwa ajili ya Uwanja huo wa kisasa wa Yanga, hivyo tunawaachia wahusika kwa ajili ya kuona kile kitakachofuata baada ya kuwaonyesha jinsi kazi hiyo itakavyoanza,” alisema Chengwei.

Aidha, Kifukwe alisema kuwa, waliwaagiza wataalamu hao tangu mwishoni mwa mwaka jana, jambo ambalo wamelifanikisha kwa kuwaita na kuzungumza nao kwa kirefu huku wakionyesha kwa vitendo mwanzo na mwisho wa ujenzi huo wa Uwanja.

“Baada ya kuonyeshwa jinsi uwanja huu utakavyokuwa utakapokamilika, tutakaa kwa pamoja kujadili gharama rasmi na kuwajulisha pia wana Yanga hatua hii, maana hii ni klabu ya wanachama na wanapaswa kufahamishwa hatua kwa hatua.

“Tutapitia wote gharama za Dola Milioni 50 kwa chagua la kwanza, Dola Milioni 40 na 30, huku tukitarajia kukutana na serikali kuangalia namna gani ramani ya Hekta 11 itatimia,” alisema Kifukwe.

Kwa mujibu wa Kampuni hiyo iliyopewa kazi ya kujenga uwanja huo wa kisasa wa Yanga, kukamilika kwake kutabadilisha kabisa eneo hilo na kuvutia zaidi kutokana na ramani na jinsi walivyoupanga uwanja huo utakaokuwa wa kuvutia.
 Huu ndio Uwanja Mpya wa Yanga utakaojengwa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group mapema mwaka huu. Mkataba wao utaingiwa mwishoni mwa mwezi wa tano.
 Francis Kifukwe kulia anapewa somo na wataalamu wa Kampuni hiyo
 Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako wa tatu kutoka kushoto mstari wa kushoto akifuatilia kwa karibu mazungumzo na kampuni watakayoipa kazi ya ujenzi wa Uwanja wao.

 Mambo ndivyo yalivyokuwa kwenye kuonyeshwa uwanja huo wa kisasa wa Yanga.
 Uwanja mpya wa Yanga utakuwa hivi.
 Picha ya pamoja kati ya viongozi wa Yanga na kampuni hiyo.
 Hapa wanaangalia uwanja utakavyokuwa katika kikao hicho.
 Hapa tumelamba dume. Duh? Simba watatukomaaaaaaaaa..

Kila la kheri Yanga katika safari hiyo ya kuhakikisha kuwa timu inakuwa na uwanja wake wa kisasa kabisa.

No comments:

Post a Comment