Rais wa BYC, Anthony Y. Beh (wa kwanza kulia) akiwa na Kocha mkuu wa BYC, Robert Lartey kwenye uwanja wa Karume leo, hawa leo ni siku yao ya kuzaliwa. |
Wachezaji wa BYC wakifanya mazoezi jana uwanja wa Azam, Chamazi |
BYC jana uwanja wa Azam |
Kocha akiangalia ufanisi wa mazoezi leo asubuki uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam |
Leo Karume mazoezi yakiendelea |
LEO ni siku ya kuzaliwa kwa viongozi wawili wa timu ya BYC ambayo ipo nchini kwa mchezo wa marudiano ya mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Azam FC.
Viongozi hao ni kocha mkuu wa BYC, Robert Lartey na Rais wa timu hiyo Anthony Beh ambayo wametimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa kwao wakiwa ugenini.
Timu hiyo jana walifanya mazoezi kwenye uwanja wa Azam uliopo Mbande na leo asubuhi wamefanyia uwanja wa Karume.
Timu hiyo inayoundwa na vijana wenye vipaji inaonekana inahitaji kushinda mchezo lakini naona Azam wana nafasi kubwa zaidi ya kushinda mchezo huo.
Hata ukiangalia ufanyaji wao wa mazoezi wanaonyesha wamekubali Azam isonge mbele kwani wenyeji wao wanawahudimia hata gari wanalotumia ni lile basi la zam kitu ambacho ni nadra sana kuona timu inayokuja kupambana nayo kukubali kutumia mali au vyakula vya wenyeji wao.
Kila la heri Azam kuiwakilisha nchi, tupo pamoja!
No comments:
Post a Comment