Tottenham leo wamepata pigo katika azma yao ya kufuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao, wakibakishwa nafasi ya 5, baada ya kuambulia sare ya 2-2 huko DW Stadium walipocheza na Wigan ambao nao sare hii haikuwanufaisha kwani bado wamebaki nafasi ya 3 toka mkiani kwenye BPL, Barclays Premier League.
Bao la kujifunga mwenyewe la Emmerson Boyce wa Wigan katika Dakika za majeruhi limewapa Tottenham sare ya Bao 2-2 na kuwaacha Wigan wakiwa bado wako nafasi hatari kuporomoka Daraja wakiwa wa 3 toka mkiani huku wakiwa Pointi 2 nyuma ya Aston Villa walio juu yao.
Hadi Dakika za majeruhi, Wigan walikuwa wakiongoza kwa Bao 2-1 kwa Bao la shuti kali la Callum McManaman ambalo liliwatoa Wigan toka Timu 3 za mkiani lakini Bao la kujifunga mwenyewe Emmerson Boyce liliwakatili na kuwarudisha mkiani wakiwa Timu ya 3 toka mwisho.
Matokeo haya pia yamewabakisha Tottenham wakiwa nafasi ya 5 wakiwa na alama 62 sawa na Chelsea ambao wako juu yao ambao pia wana hizo hizo alama 62.
Emmerson Boyce akitundika bao dakika ya 11
Emmerson Boyce wa Wigan Athletic akifanya majambo
Figueroa akitibiwa kwa haraka na daktari baada ya
kuumia ndani ya uwanja
Mchezaji Jan Vertonghen wa Tottenham Hotspur akimkwatua
Arouna Kone
Mchezaji wa Tottenham Benoit Assou-Ekotto na wa Wigan Athletic Ronnie Stam wakigombea mpira jioni hii.
BAO la kujifunga la Emmerson Boyce katika dakika za majeruhi
limeifanya Wigan Athletic kupata sare ya 2-2 dhidi ya Tottenham Hotspur na
hivyo kushindwa kujinasua kutoka kwenye shimo la kushuka daraja.
Bao maridadi la Callum McManaman liliiweka Wigan katika
nafasi nzuri ya kujitoa kwenye fungu la timu tatu za mkiani, lakini Boyce
alitibua baada ya kujifunga na kuifanya Spurs kupata sare kwenye mechi hiyo
waliyokuwa wakiongoza kwa 2-1 hadi kufikia dakika za majeruhi.
Kwa siku ya jana, ilikuwa na matamu na machungu kwa Boyce,
ambapo awali aliisawazishia Wigan kwa kichwa katika dakika ya 11, baada ya
Gareth Bale kuifungia Spurs bao la kuongoza, lakini katika dakika za majeruhi,
Boyce, alijifunga na hivyo kuwasazishia wapinzani wao, Spurs.
Pointi hizo walizogawana, zimekuwa na faida kidogo sana kwa
timu hizo, ambapo Spurs imebaki kwenye mbio zake za kushiriki ligi ya Mabingwa
barani Ulaya, wakati Wigan wakitanguliwa na timu inayoshika nafasi ya nne
mkiani, Aston Villa kwa tofauti ya pointi mbili, huku zikiwa zimebaki mechi
nne.
Stoke City imeonekana kuwa na nafasi ya kubaki kwenye ligi
hiyo msimu ujao baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Norwich City na hivyo kupanda
hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo, pointi nane zaidi ya timu tatu za mkiani.
Bao la Charlie Adam, aliyemalizia kazi ya Peter Crouch
liliisaidia timu hiyo kuiacha Norwich kwenye pointi sita kwenye nafasi yake ya
14. Everton wamerudisha matumaini yao ya kucheza michuano ya Ulaya mwakani
baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Fulham, shukrani kwa bao la kiungo wa Afrika
Kusini, Steven Pienaar.
Wakati huo huo, Marc-Antoine Fortune alifunga bao moja na
kutengeneza mawili kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu, wakati West Bromwich
Albion iliposhinda 3-0 dhidi ya Southampton, ambayo iliyobaki na wachezaji nane
uwanjani.
Mapema, mabao ya Sergio Aguero na Yaya Toure yaliisaidia
Manchester City kuinyuka West Ham United mabao 2-1 katika mechi ambayo ilikuwa
na kumbukumbu ya kiungo wa Cameroon, marehemu Marc Vivien-Foe.
Aguero alikuwa wa kwanza kuifungia Man City bao la kuongoza
kabla ya Toure kufunga na pili na Andy Carroll akiisawazishia Hammers kwa shuti
ambalo lilimshinda kipa Joe Hart kwa kumpita tobo na kuvuka mstari wa goli.
VIKOSI:
Wigan: Robles, Boyce, Scharner, Figueroa (Stam 35), Gomez (Espinoza 79), McCarthy, McArthur, Beausejour, McManaman (Di Santo 63), Kone, Maloney. Subs Not Used: Al Habsi, Caldwell, Watson, Henriquez.Booked: Gomez, Di Santo, Scharner.
Goals: Boyce 11, McManaman 49.
Tottenham: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Naughton (Assou-Ekotto 64), Parker (Lennon 73), Huddlestone, Bale, Dembele (Holtby 41), Dempsey, Defoe. Subs Not Used: Friedel, Sigurdsson, Caulker, Carroll.
Booked: Dawson.
Goals: Bale 9, Boyce 90 og.
Att: 22,326
Ref: Martin Atkinson
No comments:
Post a Comment