WAKICHEZA Mechi yao ya
kwanza bila Straika wao mkubwa, Luis Suarez, ambaye leo ameanza kutumikia
Kifungo cha Mechi 10 kwa kumuuma meno Branislav Ivanovic wa Chelsea, Liverpool
wakiwa ugenini Uwanjani St James Park, waliinyuka Newcastle Bao 6-0 katika Mechi
ya BPL, Barclays Premier League.

Mbali ya kipigo hiki kikubwa, Newcastle walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Mathiew Debuchy kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu Mbrazil Coutinho.

Matokeo haya yamewaacha Newcastle wakiwa nafasi ya 16 wakiwa Pointi 5 juu ya Wigan walio nafasi ya 18 ambao ni moja ya zile Timu za mwisho kwenye Msimamo wa Ligi na ambazo hushushwa Daraja mwishoni mwa Msimu.




VIKOSI:
Newcastle: Elliot, Debuchy, Steven Taylor, Yanga-Mbiwa, Haidara, Sissoko, Tiote (Anita 65), Cabaye, Perch (Ben Arfa 46), Gutierrez (Gouffran 46), Cisse.
Subs Not Used: Harper, Williamson, Gosling, Ameobi.
Sent Off: Debuchy (75).
Booked: Debuchy, Gutierrez, Steven Taylor.
Liverpool: Reina, Johnson, Carragher, Agger, Jose Enrique, Henderson, Gerrard (Borini 72), Lucas, Coutinho (Suso 84), Sturridge (Shelvey 84), Downing.
Subs Not Used: Jones, Coates, Skrtel, Wisdom.
Booked: Sturridge, Johnson.
Goals: Agger 3, Henderson 17, Sturridge 54, 60, Borini 74, Henderson 76.
Att: 52,351
Ref: Andre Marriner
No comments:
Post a Comment