Klaus Pagels |
HARARE, Zimbabwe
KOCHA wa timu ya Taifa ya Zimbabwe, Klaus Dieter Pagels ameita wachezaji 12
chipukizi katika kikosi chake kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Zambia
ikiwa ni mkakati wake wa kukijenga upya kikosi cha timu hiyo, kwa ajili ya
michuano ya COSAFA.“Awali nilipanga kuita kikosi cha vijana, lakini nimeona kwamba kuna haja ya kuiimarisha timu yangu ya kikosi cha kwanza, hasa kwa kuona kwamba Zambia wameita wachezaji wao wote nyota, naupa umuhimu mkubwa mchezo huu na ndiyo utanisaidia kuipanga upya timu kwa ajili ya michuano ya COSAFA na ile ya kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia,” alisema Pagels.
Alisema wako katika mchakato wa kuijenga timu ya wachezaji wa ndani ambayo pia itashiriki michuano ya CHAN, na kwamba wachezaji wengi wanaounda kikosi cha Zimbabwe wanatoka katika timu za ndani hivyo ameweka mkazo kwa wachezaji hao.
"Nimeita wachezaji 12 ambao hawajawahi kuichezea timu ya taifa, hii ni kutaka kuwapa uzoefu najua kwamba Zambia wamefanya hivyo pia na huu ndiyo mfumo wa kisasa wa kukuza vipaji vya wachezaji wa timu ya taifa,” alisema.
No comments:
Post a Comment