Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, April 29, 2013

DUNGA AIBEBA TESKER KUILAZA STIMA

Dunga
NAIROBI, Kenya
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka nchini Kenya, timu ya Tusker wamezinduka baada ya juzi Ismail Dunga kuipa timu hiyo ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Western Stima  katika uwanja wa Afraha.
Hata hivyo haikuwa ushindi rahisi kwa Tusker, kwani muda mwingi walijikuta wakishambuliwa na Stima na kwamba washambuliaji wa Stima Dennis Onkangi, Fred Shimonyo na Job Omuse wanapaswa kutwishwa mzigo wa lawama kwa kushindwa kuipa timu yao ushindi kutokana na kupoteza nafasi nyingi.
Omuse alipata nafasi mbili za wazi, lakini alipiga mpira nje huku wenzake nao wakiwa wanapoteza nafasi mara kadhaa katika kipindi cha kwanza, ambacho timu yao ilicheza vizuri sana na kutawala kwa sehemu kubwa.
Kipindi cha kwanza ndiyo kilikuwa kigumu zaidi kwa Tusker, kwani ilikuwa katika wakati mgumu, lakini kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko kwa kumuingiza Joshua Oyoo hatimaye walizinduka na Oyoo alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Stima.
Iliwalizimu Tusker kusubiri hadi dakika ya 73 wakati ambapo Oyoo alipowahandaa mabeki na kutoa pasi kwa Dunga aliyekuwa ndani ya eneo la hatari na kisha kuukwamisha mpira wavuni. Kwa ushindi huo Tusker imepanda hadi katika nafasi ya 12 ya msimamo wa ligi hiyo wakati Stima imebaki katika nafasi ya tisa kwa kuwa na pointi 11.

No comments:

Post a Comment