Cesar, mwenye Miaka 33 na Mchezaji wa Kimataifa wa Brazil, alijiunga na QPR kutoka Inter Milan ya Italy mwanzoni mwa Msimu na tayari ameshaidakia QPR mara 26 lakini ameshindwa kuzuia Timu hiyo isiwe hatarini kushushwa Daraja kwani ipo nafasi ya Pili toka mkiani na huenda ikaporomoka Wikiendi hii ikiwa matokeo yatakuwa mabovu kwao.
Picha hiyo ya Cesar na Jezi ya Chelsea ilipigwa akiwa pamoja na Beki wa Chelsea, David Luiz, ambaye pia ni Mchezaji wa Brazil, wakisheherekea Siku ya Kuzaliwa ya Luiz.
QPR imethibitisha kuhusu kuwepo kwa Picha hiyo na kutamka suala hilo litashughulikiwa ndani ya Klabu.
JEZI YAMTIA MATATANI CESAR!!
Wakisheherekea Siku ya Kuzaliwa ya Luiz.
Marko Marin na Luiz
No comments:
Post a Comment