|
Wachezaji wa Jeshi Stars wakishangilia ushindi na familia zao |
|
Nahodha wa Jeshi Stars akikabidhiwa kikombe cha ubingwa wa mashindano ya muungano na Naibu Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni, Juliana Yassoda |
|
Nahodha wa Magereza akipokea kikombe cha mshindi wa pili toka kwa Naibu Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni, Juliana Yassoda |
|
Mchezaji wa Magereza akirudisha mpira kwa wapinzani wao Jeshi Stars |
|
Wachezaji wakipeana fair play baada ya mchezo kumalizika |
|
Magereza stars |
|
Jeshi Stars |
TIMU ya
Jeshi Stars wanawake jana walifanikiwa kutwaa kombe la Muungano baada ya
kuifunga Magereza seti 3 kwa 0 kwenye
mchezo wa wavu uliochezwa Uwanja wa ndani wa Taifa.
Mchezo huo
ulikuwa wa upande mmoja ulishuhudia kila seti Jeshi wakimaliza wakiongoza.
Jeshi
walishinda kwa 25 kwa 20, 25 kwa 17 na 25 kwa 19 na kujichukulia kombe la
Muungano kirahisi.
Zawadi ya
mchezaji bora ilikwenda kwa Christina Msuya na Yasinta Remmy wa Jeshi Stars na
kupewa zawadi ya mpira mmoja mmoja na Hellen Mwegoha wa Magereza ambaye na pia alipewa mpira.
No comments:
Post a Comment