Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, April 29, 2013

GARETH BALE AWA MCHEZAJI BORA WA AFP





KIUNGO wa klabu ya Tottenham Hotspurs Gareth Bale amekuwa mchezaji wa tatu kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wakubwa na wachezaji wanaochipukia kwa msimu mmoja

Tuzo hizo hutolewa na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa nchini Uingereza. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 23 ambaye pia alishinda tuzo ya wakubwa mwaka 2011, amefunga mabao 19 katika ligi msimu huu na kuwa nyuma ya kinara wa mabao Robin van Persie mwenye mabao 25 na Luis Suarez mwenye mabao 23.

 Akikabidhiwa tuzo hiyo Bale amesema ni heshima kubwa kwake kunyakuwa tuzo hizo mbili muhimu na kushukuru wapiga kura kwa kutambua mchango wake haswa ikizingatiwa kumekuwa na majina makubwa mengine katika orodha iliyokuwepo.

Bale anaungana na wachezaji wengine walioshinda tuzo ya wakubwa mara mbili ambao ni Cristiano Ronaldo, Thierry Henry, Alan Shearer and Mark Hughes wakati walioshinda tuzo zote mbili kwa mwaka mmoja ni Ronaldo mwaka 2007 na Andy Gray mwaka 1977.

No comments:

Post a Comment