RAIS wa Shirikisho la Soka Barani
Afrika-CAF, Issa Hayatou amechaguliwa tena bila kupingwa kuendelea kushika
wadhfa huo kwa kipindi cha miaka mingine minne. Katika uchaguzi huo Danny Jordaan
ambaye alijitengenezea jina kubwa kimataifa baada ya kuandaa michuano ya Kombe
la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010 ameshindwa kwa mara nyingine kupata
nafasi ya ujumbe katika kamati ya utendaji ya CAF. Jordaan alishindwa na mgombea kutoka
Madagascar aliyetumia jina moja la Ahmad katika uchaguzi hiyo ikiwa mara ya pili
kukosa nafasi hiyo nyeti baada ya mara ya kwanza kugaragazwa katika mkutano
uliofanyika nchini Sudan miaka miwili iliyopita. Katika mkutano huo uliofanyika jijini
Marrakech nchini Morocco aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la
Soka la Dunia-FIFA Amadou Diakite alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji
ya CAF. Diakite alifungiwa
na FIFA kwa miaka miwili Novemba mwaka 2010 baada ya kutuhumiwa kupokea rushwa
katika skendo ya kununua kura uliozunguka nchi zilizopewa uennyeji wa kuandaa
michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022. Shirikisho hilo linatarajia kufanya
mkutano mwingine nchini Brazil mwaka 2014 lakini kutakuwa hakuna uchaguzi tena
mpaka mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment