Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole
Mzee` Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee marufu wa Klabu ya Dar es salaam Young
Africans (YANGA) ambaye amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza
majeraha kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini
Dar es salaam. Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya
usoni na mikononi. Hadi jana hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete
amempa pole kwa maumivu aliyoyapata na kumtakia apate nafuu ya haraka. PICHA NA
IKULU
No comments:
Post a Comment