Aliyekuwa katibu wa shirikisho la soka nchini TFF Fredrick Mwakalebela akimkabidhi kombe la ubingwa wa soka Iringa mjini nahodha wa timu Mshindo pamoja na fedha taslimu shilingi laki tano kufuatia kutwaa ubingwa wa ligi ya Iringa mjini katika uwanja wa Samora. Timu ya magereza ilishika nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi laki tatu. |
Mwakalebela akitoa neno la kwa mashabiki wa soka wa Iringa mjini wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa ligi ya Iringa Mjini jioni ya leo., |
Hizi ni baadhi ya zawadi kwa washindi. |
Hapa akizikagua timu za Mshindo na Magereza. |
TIMU ya Mshindo FC jana iliibuka mabingwa wa ligi daraja la
nne wilaya ya Iringa Mjini baada ya kuifunga Magereza mabao 3-2 na kufanikiwa
kuondoka na Kombe na kitita cha shilingi laki tano kwenye mchezo uliochezwa
uwanja wa Samora mjini Iringa.
Mchezo huo ambao ulivuta hisia za mashabiki wa mji wa Iringa
ulishuhudia Mshindo wakienda mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na
Abdallah Mativila dakika ya 27 na 30
Kipindi cha pili kilianza kwa timu kufanya mabadiliko na
Magereza walipata bao kupitia kwa John Ngairo dakika ya 65 bao ambalo halikudu muda mrefu kwa Abdallah
Mativila aliongeza bao la tatu kwa Mshindo dakika ya 78 na John Ngairo wa
Magereza aliongeza bao la pili dakika ya 80.
Magereza ambao ni washindi wa pili waliondoka na zawadi ya
lakini tatu na mshindi wa tatu Mtwivila City walizawadiwa shilingi laki mbili
Mlinda lango bora Sunday Mwakasala alipewa zawadi ya
shilingi elfu hamsini wakati mfungaji bora Kasim Mataka alifunga mabao 18 alipewa
shilingi elfu 80. Wakati timu yenye nidhamu, Uhuru FC ilipata laki moja.
Akizungumza na Mtanzania kwa njia ya simu toka Iringa,
Katibu wa chama cha Soka Rashid Shungu alisema anashukuru Ligi imemalizika
salama na mshindi amepatikana.
No comments:
Post a Comment