Luiz Felipe Scolari anarudi tena Stamford Bridge, mahala ambako alikaa Miezi 7 kama Meneja wa Chelsea kabla kutimuliwa, safari hii akiwa Kocha wa Brazil ambayo Jumatatu itacheza Mechi ya Kirafiki na Russia.
Scolari alikuwa Meneja wa Chelsea kuanzia Julai 2008 hadi Februari 2009 na kutimuliwa na Mmiliki wa Klabu Mrusi Roman Abramovich baada ya mwendo mbovu.
Kikosi cha Brazil kitakachocheza na Russia huenda kikawa na Wachezaji watatu wa Chelsea, David Luiz, Ramires na Oscar, lakini ni wazi Abramovich atakuwa akiishangilia Nchi yake Russia kwenye Mechi hiyo ya kwanza ya Kimataifa, kati ya Nchi na Nchi, kuchezwa Stamford Bridge katika Miaka 67.
Hii itakuwa ni Mechi ya 3 kwa Scolari tangu achukuwe wadhifa huo na hadi sasa hajashinda hata Mechi moja baada ya kufungwa 2-1 na England na kisha juzi Ijumaa kutoka sare 2-2 na Italy huko Geneva, Uswisi.
Scolari, mwenye Miaka 64, ndie alieiongoza Brazil kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 2002 na amepewa wadhifa wa kuiongoza tena Nchi yake ili watwae tena Ubingwa wa Kombe la Dunia kwenye Fainali zitakazochezwa Brazil Mwaka 2014.
Akiongelea Timu yake, Scolari amesema: “Kwangu mimi naona yapo maendeleo. Bado tunajaribu kuweka staili yetu sawa. Lakini nimeipenda Timu na jinsi inavyojiendesha.”
Kwa sasa, Scolari amebainisha kuwa anajaribu Wachezaji wengi kabla hajapata Kikosi kitakachocheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yatakayochezwa huko Brazil na wao kuanza Juni 15 kwa Mechi na Japan.
You couldn't make it up: Fabio Capello in front of a Chelsea logo wearing a blue tracksuit
At the Bridge: Capello took a training session for his squad at Chelsea's ground
All together now: Capello talks to his Russia players ahead of the glamour friendly
Old haunt: Yuri Zhirkov played at Chelsea for two seasons but struggled to make a lasting impact
View from the Bridge: Russia's players prepare to face the likes of Neymar, Kaka and Oscar
No comments:
Post a Comment