TIMU ya Yanga leo imeifunga timu ya African Lyon mabao 4-0 kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabao ya Yanga yalitiwa kimiani na Jerryson Tegete aliyefunga mawili, Didier Kavumbagu na Nizar Khalfan akahitimisha karamu ya mabao.
Matokeo mengine Kager Sugar wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Kaitaba wameifunga Coastal Union bao 1-0 na Toto African ya Mwanza wakiwa nyumbani walitoshana na nguvu na Polisi Morogoro kwa kufungana mabao 2-2.
Mtibwa Sugar wametoka suluhu na Ruvu shooting baada ya mchezo uliopita kufungwa mabao 4-1 na Azam, FC.
No comments:
Post a Comment