Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, February 21, 2013

TBL YAKABIDHI BASI KWA TAIFA LEO, YASISITIZA LITUMIKE KWA MANUFAA YA SOKA TU


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Robin Goetzsche (wa pili kushoto) akikabidhi funguo kama ishara ya kukabidhi basi la Taifa Stars kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Leodgar Tenga (wa tatu kushoto) wakati Kilimanjaro Premium Lager ilipokabidhii basi hilo leo makao makuu ya TBL Jijini Dar es Salaam.

Kocha Kim Poulsen na Erasto Nyoni wakishuka baada ya kuliona basi lilivyo huko ndani

 
  Rais wa TFF, Leodgar Tenga akisaini mpira
                                                      Basi lililotolewa na  (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro
                                                        Mdau akiwa amejichora rangi za bendera ya Taifa
                                     
                                                   Kocha Kim akisaini mpira
Wakaguzi wa ukanda wa Afrika wa brand ya bia ya Kilimanjaro
 


KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro ambao ni wadhamini wa timu ya taifa ya (Taifa Stars) leo wamekabidhi rasmi basi la timu hiyo yenye dhamani ya zaidi ya million 200.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa basi hilo lina uwezo wa kubeba abiria 51, uwezo wa injini ni 300 HP Cummins na kumeza lita 800 za mafuta.
Kavishe alifafanua kuwa TBL limenunua basi hilo ikiwa ni sehemu ya ufadhili kama ilivyoaishwa katika mkataba baina ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kampuni hiyo.

“Imeshatimia miezi 10 tangu toka TBL ilipoanza kufadhili Taifa Stars na malengo yetukama wadhamini ni kuiona timu ikipata ushindi uwanjani na kuongeza sifa ya timu na tumerithika na matoke,”Alisema.

Alisema kuwa TBL itaendelea kusaidia timu ya taifa na hivyo kupandisha kiwango cha soka nchini ili baadae waweza kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika na baadae kombe la dunia.

Nae Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga alihaidi kulitunza basi hilo kwa mafanikio ya timu hiyo ya Taifa ambayo kwa sasa inafanya vema katika michezo mbalimbali.
Tenga alisema kuwa ujio wa basi hilo ni ishara nzuri ya kuifikisha timu hiyo kwenye mafanikio zaidi

 

No comments:

Post a Comment