Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, February 3, 2013

KASI YA YANGA YAPOZWA NA MTIBWA SUGAR.

Haruna Niyonzima akikabiliana na Jamali Mnyate wa Mtibwa sugar.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga waliohudhuria mchezo huo wakiwa wamekata tamaa baada ya kuwa nyuma kimatokeo mpaka dakika ya 86 ya mchezo huo.
 Mabingwa wa soka Afrika Mashariki na kati Yanga ambao pia ndio vinara wa ligi hiyo hii wameponea chupuchupu kupote mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ukiwa ni mchezo wa mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania bara pale walipolazimika kusubiri mpaka zikiwa zimebakia dakika 4 za muda wa kawaida kupata bao la kusawazisha.
Bao lililo iokoa Yanga limefungwa na Hamisi Kiiza kunako dakika ya 84 ya mchezo baada ya kupokea pasi ya Saidi Bahanuzi kutoka wingi ya kulia.
Licha ya kutawala mchezo huo kwa sehemu kubwa, bado umakini mdogo na utulivu wa washambuliaji wa Yanga waliokuwa wakiongozwa na Jerson Tegete , Kiungo Haruna Niyonzima, Simon Msuva na Didier Kavumbagu na baadaye kuingia Hamisi Kiiza na Saidi Bhanuzi iliichelewesha Yanga kupata bao la mapema la kusawazisha.
Mtibwa waliaandika bao la uongozi kupitia kwa Shabani kwa kichwa baada ya kupokea mpira wa kona  kutoka kwa Issa Rashidi dakika moja kabla ya mapumziko.
Mtibwa iliyokuwa ikiunganishwa na Shabani Nditi, Shabani Kisiga na Rashidi Gumbo kabla ya kutolewa ilikuwa ni kama imeridhika na bao la Kisiga na hivyo kutumia sehemu kubwa ya kipindi cha pili kujihami hali iliyopelekea Yanga kupanga mashambulizi kupitia pembeni kwa Msuva na Haruna Niyonzima huku Jerson Tegete na Hamisi Kiiza wakipokea mipira mingi sehemu ya kati ya ushambuliaji na kuwapa kazi ya ziada walinzi Salum Swedi, Saidi Mkopi Rajabu Mohamed na Issa Rashidi kuokoa mipira mingi katika dakiki 20 za mwisho wa mchezo.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kupungunzwa kasi yake katika msimamo wa ligi ambapo sasa ina ongoza kwa tofauti ya alama 3 mbele ya Azam fc yenye alama 30 na Yanga ikiwa na alama 33.

No comments:

Post a Comment