Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, February 3, 2013

MALI YAUNGANA NA GHANA KUTINGA NUSU FAINALI YA FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA.


Wachezaji wa timu ya taifa ya Mali wakishangilia baada ya kufanikiwa kuifunga Afrika kusini kwa njia ya penati katika mchezo wa pili wa robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika.
 Mlinda mlango wa Mali Soumaila Diakite aliibuka shujaa usiku wa jana baada ya kufanikiwa kudaka penati mbili ambazo zilipelekea matokeo ya ushindi wa penati 3-1 dhidi ya waandaji wa fainali za mataifa ya Afrika Afrika kusini na kuivusha Mali mpaka katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Kabla ya penati hizo kupigwa, mchezo huo uliingia katika dakika 30 za nyongeza matokeo yakiwa ni 1-1 na baadaye dakika 120 kumalizika bila kupatikana mbabe.

Tokelo Rantie aliwapa uongozi Afrika kusini kwa bao la dakika ya 31 ya mchezo ambao umepigwa katika dimba la Mabhida kabla ya nahodha Seydou Keita wa Mali kusawazisha dakika ya 12 ya kipindi cha pili.
Siphiwe Tshabalala alianza kuandika bao kwa penati yake nzuri ya kwanza kabla ya Cheick Diabate kufunga penati ya kwanza kwa Mali. Furman na penati zao zilidakwa na mlinda mlango wa Mali Diakite ilihali penati za Adama Tamboura na Mahamane Traore wakifanikiwa kufunga penati zao kabla ya Majoro wa Afrika kusini kupiga pembeni penati yake na kufanya matokeo ya penati kuwa 3-1 hivyo Mali kufanikia kufuzu.

GHANA 2 CAPE VERDE 0
Wachezaji wa Ghana wakishangilia baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika kufuatia kuichapa Cape Verde kwa mabao 2-0 mchezo uliopigwa katika mji wa Port Elizabeth.

Mubarak Wakaso aliyeingia uwanjani akitokea benchi alifanikiwa kufunga mabao yote katika kipindi cha pili bao la kwanza akifunga kwa njia ya mkwaju wa penati na bao la pili akifunga katika dakika moja kabla ya mchezo kumalizika baada ya mlinda mlango wa Cape Verde Josimar Vozinha kuliacha goli na kwenda kushambulia wakati kona ikipigwa.

No comments:

Post a Comment