Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 11, 2013

DSTV YAONYESHA FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA LIVE NA MASHABIKI ZANZIBAR JANA USIKU

Kwa zaidi ya wiki tatu zilizopita, kuanzia Januari 19, 2013 mpaka Februari  10, 2013 mashabiki wa soka barani Afrika na duniani kote walikuwa hawabanduki katika viti vyao au sofa kwa ajili ya kutizama mashindano makubwa kabisa ya soka barani Afrika ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika mashindano ambayo kwa kizungu yanajulikana kama Orange Africa Cup Of Nations.
 
Wenyeji wa mashindano ya mwaka huu walikuwa Afrika Kusini. Jumla ya mechi 32 zilichezwa na zote zilionyeshwa Live bila chenga kupitia channels za SuperSport zinazopatikana kupitia DStv, wakongwe wa digitali.
 
Wakati wa fainali, DStv kupitia kampuni mama ya MultiChoice Tanzania walijumuika na mashabiki wa soka na wadau mbalimbali visiwani Zanzibar katika viota vya Gymkhana Club na Mtoni Marine. Huko palikuwa na special screening ya mchezo huo wa fainali ambapo Nigeria waliibuka mabingwa (kwa mara ya tatu sasa) baada ya kuwalaza Burkina Faso kwa goli 1-0
 
Kwa mapana na marefu umekuwa msimu wa kufurahi na marafiki na pia kutizama jinsi ambavyo kabumbu linazidi kutamba kama mchezo unaopendwa zaidi sio tu Afrika bali duniani kote.
Picha moja ni sawa na maneno elfu moja. Sehemu ya umati wa mashabiki wa soka Zanzibar wakifuatilia kwa makini mchezo wa fainali kati ya Nigeria na Burkina Faso wakati wa special screening ya fainali hiyo iliyowezeshwa na DStv ndani ya Gymkhana Club.
Experience The Spirit Of Africa- wadau wa soka ndani ya kiota cha Mtoni Marine wakiwa wenye tabasamu wakati wa fainali ya AFCON 2013.

Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa makini mtanange wa fainali ndani ya Mtoni Marine.Uwapo Zanzibar na unataka kuangalia michezo kama huu wa fainali ya AFCON 2013, Mtoni Marine ni sehemu inayohusika. Kila kona pametapakaa TV Screen ambazo zote, Live bila chenga hurusha matukio ya michezo kupitia DStv, wakongwe wa digitali.
Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu(kushoto) akiwa na wakurugenzi wa Island Promotions, Adelina Ngalo(katikati) na Ameir Kombo.
Macho yote katika screen. Mchezo wa fainali unaendelea-Gymkana Club.
Mkurugenzi wa Island Promotions,Ameir Kombo, akisaidia zoezi la maswali na majibu kuhusiana na michuano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa Afrika-AFCON 2013. Kushoto kwake ni Mohamed kutoka IBS-, mahali ambapo unaweza kupata huduma za aina zote zinazohusiana na DStv.
Mbali na kufurahia Soka, mashabiki mbalimbali walijishindia zawadi mbalimbali kutoka DStv.
Ni SuperSport, Ni Zanzibar, Ni DStv.
Sehemu ya umati wa mashabiki wa soka waliofurika kushuhudia Live mchezo wa fainali ya AFCON 2013.
Baadhi ya washindi wa zawadi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na DStv wakati wa special screening ya fainali ya Africa Cup Of Nations wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa DStv akiwemo Meneja Masoko wa MultiChoice,Furaha Samalu

No comments:

Post a Comment