Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 11, 2013

ASHANTI UNITED YAICHAPA TRANSIST CAMP 3-2


TIMU ya Ashanti imeendeleza wimbi la ushindi baada ya juzi kuwafunga maafande wa Transit Camp mabao 3-2 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulikuwa wa ushindani lakini washambuliaji wa Ashanti waliizidi ujanja beki ya Transit Camp na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.

Mabao ya Ashanti yaliwekwa kimiani na Habibu Shaban dakika ya 27 na Jerome Lambele alifunga dakika ya 33 kwa kichwa baada ya kupokea krosi safi toka kwa Emanuel Lusajo.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko, wakati Transit camp wakijipanga vema Ashanti waliongeza bao kupitia kwa Emanuel Lusajo dakika ya 68.

Baada ya Ashanti kuongeza bao la tatu Transit Camp walicharuka na kuanza kuliandama lango la Ashanti na kufanikiwa kujipatia mabao mawili ndani ya dakika 6 kupitia kwa Kasim Mohamed dakika ya 82 na Mohamed Ussi dakika 88.

Kwenye uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani Polisi Dar es salaam iliifunga Moro United mabao 2-0 na jijini Mbeya, wenyeji Mbeya City waliifunga Polisi Iringa mabao 2-0.

JKT Mlale wao walitoshana nguvu na Kurungezi ya Njombe baada ya kufungana mabao 2-2 mchezo uliochezwa uwanja wa Majimaji mjini Songea.

No comments:

Post a Comment