TANZANIA imepanda kwa nafasi sita kwenye
viwango vya ubora vinavyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutoka nafasi
ya 130 iliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 124.
Timu tano bora kwa upande wa dunia zote
zimebaki katika nafasi zao waliokuwepo mwezi uliopita ambapo wanaongoza na
Hispania inayoshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na nchi za Ujerumani, Argentina,
Italia na anayefunga orodha ya tano bora ni Colombia.
Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast
imeendelea kuongoza huku ikishika nafasi ya 14 kwa upande wa dunia, ikifuatiwa
na Algeria inayoshika nafasi ya pili pamoja na kuporomoka kwa nafasi tatu mpaka
ya 24 kwa upande wa dunia.
Nchi zingine za Afrika ni Mali
iliyobaki katika nafasi yake ya 25 waliyokuwepo mwezi uliopita wakifuatiwa na
Ghana waliopanda kwa nafasi nne mpaka nafasi ya 26 na tano bora kwa upande wa
Afrika inafungwa na mabingwa wa Afrika Zambia ambao wamekaa katika nafasi ya 39
baada ya kuanguka kwa nafasi tano.
No comments:
Post a Comment