Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 22, 2013

SIMBA YAUNDA KAMATI ZAKE NDOGO


Baada ya Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage kuvunja kamati zote ndogo katika klabu hiyo, klabu hiyo imetangaza majina ya kamati mpya ambazo zinatakiwa kuanza kazi mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.

Rage alivunja kamati hizo baada ya kumalizika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara na kutangaza kuunda kamati nyingine kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili.
Katika mabadiliko hayo kamati ambayo kiongozi wake ameweza kurudi katika nafasi yake ni Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Godfrey Nyange ‘Kaburu’ katika kamati ya Fedha.
Afisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema alitangaza kamati hizo kuwa katika kamati ya Ufundi ambayo ilikuwa inaongozwa na Ibrahimu Masoud ‘Maestro’ sasa itaongozwa na Damian Manembe.

Hata hivyo katika kamati hiyo ya Ufundi Rage amechagua wajumbe wengi ambao walishawahi kuchezea Simba ambao ni Yusuph Macho, Zamoyoni Mogela, John ‘Del Bita John, Shaaban Baraza, Said Tully na Khalid Abeid.

Alisema Kwenye Kamati ya fedha Mwenyekiti wake ataendelea kuwa Godfrey Nyange ‘Kaburu’ huku Makamu wake akiwa Rahma Al Kharoos ambaye ndiye aliyeipeleka Simba kambi ya wiki mbili Oman huku Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe na Mbunge wa Iramba Juma Mnkamia wakiingizwa katika kamati hiyo .

Kamati ya Mashindano ambayo ilikuwa chini Joseph Itang’ala ‘Kinesi ambaye amepelekwa kwenye kamati ya vijana sasa itakuwa ikiongozwa na Sweddy Mkwabi huku kwa iande wa kamati ya programu ya vijana itakuwa ikiongozwa na Ibrahim Masoud ‘Maestro’na Makamu wake akiwa ni Ruge Mutahaba.

Kamwaga alisema uteuzi huu wa wajumbe unaanza mara moja na wenyeviti wa kamati hizo wamepewa nguvu ya kuitisha vikao vya kamati zao mapema iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment