Hapa wakipewa maelekezo na PR wa shughuli hiyo,kabla ya kuanza kwa mazungumzo na Vyombo vya Habari ,katika mkutano wa vyombo vya habari vilivyofanyika Jijini Arusha. | . |
**********************
“Sisi kama wadau wakubwa na wazalendo wa michezo
Tanzania ,tumeamua kuanzisha tukio hili la harambee, kupitia
kukimbia mbio za kupokezana vijiti (RELAY MARATHON) , ili kuchangisha pesa ya
kuanzisha kiijiji cha kitaifa cha Michezo nchini Tanzania .
Pia kijiji hicho cha michezo Tanzania kitaitwa
“John Stephen Akhwari National Sports Village” ,kwa heshima ya mwanariadha huyo
wa kimataifa alieiletea sifa nchi ya Tanzania kwa kukimbia bila kukata tamaa
,hata aliposhindwa alidiriki kusema “Nchi yangu haijanituma kuja kuanza
mashindano: bali kumaliza Mashinadano.
Pia baada ya kuona michezo mingi Tanzania imekosa
vituo vyenye hadhi ya kimataifa vya kufanyia mazoezi yenye ubora wa
kimataifa,ili kupata medali ndani na nje nchi yetu.
Hivyo tukakaa na baadhi ya wanariadha wazalendo
nchini kama vile,Phaustin Baha na Rogart John Stephen ,ili tufanye tukio hili la
kihistoria ambalo hakuna mwingine aliewahi kujaribu kulifanya “alisema Wilhem
Gidabuday.
“Mashindano hayo yatakuwa ya mbio za kupokezana
vijiti yaani (RELAY MARATHON) kuanzia Magogoni jijini Dar es Salaam (IKULU) na
kumalizia jijini Arusha (Sheikh Amri Abeid) kupitia barabara kuu itokayo Dar es
Salam hadi Arusha, yenye takribani kilomita zisizopungua mia saba (700 Km). Mbio
hizo zitahusisha wanariadha wa tano maarufu na wazalendo na ambao wamewahi
kukimbia na kuiletea nchi yetu sifa kimataifa”.aliongeza Bw.
Gidabuday
Malengo ya Mbio hizi ni:
Moja; kuwezesha kuanzisha kijiji cha michezo
Tanzania kulingana na jeografia ya nchi yetu ilivyo, kuwa na maeneo ya nyanda za
juu kaskazini na kusini ambamo hali ya hewa inaruhusu michezo mingi kufanyika
ikiwemo mchezo wa riadha. hili litasaidia kupata wanamichezo wazuri na wenye
lengo la kuiletea sifa na medali nchi yetu kitaifa na kimataifa na kuongeza
ajira kwa wanamichezo wetu.
Pili ; kwa kuwa Raisi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. Jakaya Kikwete ni msikivu ,anapenda michezo na alitambua mchango
mkubwa wa mwanariadha mkongwe Bw. John Stephen Akhwari na kumpa Tuzo ya miaka 51
ya Uhuru wa Tanzania ,ndipo tukapendekeza kijiji hiki cha michezo kiitwe John
Stephen Akhwari, ila kijiji hiki ni mali ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mashindano haya yanatarajiwa kufanyika kabla ya
mwezi wa sita mara tu tutakapowapat a wahisani,Serikali na wadau wengine wa
michezo kujitokeza na kuwezesha jambo hili kutimia . hivyo tunaiomba serikali
,wadau mbalimbali wa michezo nchini pamoja na wahisani wajitokeze ili kutimiza
lengo hili la kitaifa la kuanzisha kijini cha michezo cha John Stephen
Akhwari.
Mwisho, Mwaka ujao wa 2014 tunatarajia kukimbia mbio
zingine kutoka Bagamoyo hadi ujiji, katika miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, lengo ni kuhamasisha na kuchangisha pesa za ujenzi wa kituo hicho cha
kimataifa.
No comments:
Post a Comment