Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 22, 2013

IVORY COAST YAIBANJUA TOGO 2-1,GERVINHO AITAKATIISHA IVORY

Ivory Coast imeanza kampeini yake ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa kuilaza Togo kwa magoli mawili kwa moja katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi D.
Ivory Coast ilipata bao lake la kwanza kunako dakika ya nane kupitia kwa mchezaji Yaya Toure na kwa mara nyingine, wachezaji hao wa Ivory Coast wanatafuta fursa ya kutwaa kombe hilo ambalo liliwaponyoka mwaka uliopita.Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba, analiongoza tena timu hiyo, kwa fainali hizo ambazo ndizo za mwisho atakazoshiriki. Licha ya wengi kuipa timu hiyo ya Ivory Coast nafasi kubwa ya kushinda mashindano ya mwaka huu, The Elephants hawakucheza mechi ya kusisimua katika kipindi cha kwanza.
Mara ya Mwisho Ivory Coast, ilishinda kombe hilo ni mwaka wa 1992.



Togo nayo inaongozwa na mshambulizi wa Tottenham, Emmanuel Adebayor.
Dakika ya 44, Yahya Toure, nusura afunge bao la pili, lakini mkwaju wake uligonga mlingoti.
Ushirikiano kati ya Didier Drogba, Yahya Toure and Gervinho umeonekana kuwa nguzo ya timu hiyo ya Ivory Coast.
Dakika moja baadaye Togo ikasawazisha baada ya walinda lango wa Ivory Coast kufanya masihara, kwenye eneo la hatari.
Kufikia wakati wa mapumziko timu hizo mbili zilikuwa zikitoshana na nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.
Lakini katika kipindi cha pili, Ivory Coast iliimarisha mashambulizi yake na kunako dakika ya 87, ivory coast ikapata bao lake la pili kupitia kwa mchezaji Gervinho.
Ivory Coast sasa inaongoza kundi hilo la alama tatu huku Togo ikiwa bila alama yoyote.
Kinyume na ilivyotarajiwa, mechi hiyo iligeuka na kuwa maonyesho ya nguvu, baina ya wachezaji kadhaa wanaoshiriki katika ligi mbali mbali za kulipwa na mara nyingi ilikuwa kati ya Kolo Toure na Adebayor na Vincent Bossou na Didier Drogba ambao walifanya makosa mengi na hivyo kuhujumu mtiririko wa mechi hiyo.
Mechi ya pili ya kundi hilo kati ya Tunisia na Algeria itaanza mwendo wa saa tatu za usiku majira ya Afrika Mashariki.

Gervinho akishangilia kivyake baada ya kuiokoa Ivory Coast usiku huu.
Vinara wa EPL Kolo Toure (kushoto), Cheick Tiote (kulia) na Emmanuel Adebayor (kati) wakigombea mpira usiku huu kwenye AFCON 2013

Yaya Toure (katikati) akipongezwa na wenzake

Gervinho akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la ushindi na hapa anabusu uzi

Shabiki wa Togo kushoto na kulia ni shabiki wa Ivory Coast akipuliza "vuvuzela"

No comments:

Post a Comment