Chama cha netiboli nchini (CHANETA) kimesema kitatoa adhabu kwa
viongozi wa mikoa ambayo haijaitisha uchaguzi wa viongozi bila ya kutoa
sababu za msingi.
Kaimu Katibu Mkuu wa CHANETA, Rose Mkisi amesema mikoa hiyo tayari
viongozi wake wamemaliza muda wao lakini wanashindwa kuitisha uchaguzi
wa viongozi.
Mkisi aliitaja mikoa hiyo ambayo iko hatarini kupewa adhabu na CHANETA
ni pamoja na Tanga, Manyara, Arusha,Kilimanjaro Mara, na Rukwa.
Mikoa mingine ambayo bado haijaitisha chaguzi zake ni pamoja na Dodoma, Tabora, Shinyanga, Iringa,Kagera, na Kigoma.
"Tunaomba mikoa hiyo ifanye chaguzi ili kufanikisha CHANETA kuitisha
uchaguzi mkuu, bila ya kufanya hivyo itapewa adhabu," aliongeza Mkisi.
Mkisi aliongeza mikoa hiyo ndio chanzo kikubwa cha CHANETA kuchelewa
kuitisha uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wapya
watakaokiongoza chama hicho kwa muda wa miaka minne.
Mkisi aliitaja mikoa ambayo tayari imefanya chaguzi zake ni kuwa ni
pamoja na Dar es Salaam, Mwanza, Lindi, Mtwara,Morogoro, Ruvuma, Mbeya,
na Singida.
Alisema wakitekeleza zoezi hilo mapema itakuwa rahisi kwa CHANETA kuanza
harakati za uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi wapya wa chama hicho.
Wakati huo huo, Mkisi aliwataka wachezaji wa timu ya taifa ya netiboli
kujitokeza mazoezini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya kimataifa
yaliyopo kwenye kalenda ya mwaka.
mazoezi hayo kwa sasa yatakuwa yanakwenda na kurudi nyumbani chini ya
makocha Mary Protasi na Mary Waya kwa ajili ya kuiandaa timu hiyo na
mashindano ya kimataifa yaliyopo kwenye kalenda ya mwaka. Aliongeza
wachezaji wote wanatakiwa kuhudhuria mazoezi hayo ili iwe rahisi kwa
kocha kuweza kuchagua kikosi cha kwanza cha timu hiyo
kitakachoiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment