Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, January 13, 2013

YANGA KUREJEA ALFAJIRI KESHO BAADA YA ZIARA YAO NCHINI UTURUKI

TIMU ya Young Africans iliyokuwa imeweka kambi ya mafunzo kwa muda wa wiki mbili inatarajiwa kuondoka majra ya mchana mjini Antalya - Uturuki kupitia Istambul ambapo inatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa JNIA Dar es salaam majira ya saa 10 kasorobo kwa saa za Afrika Mashariki.
Young Africans ambao ni Mabingwa mara 23 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara na Bingwa mara tano (5) wa kombe Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati iliweka kambi ya mafunzo katika mji wa Antalya kwa muda wa takribani siku 14 ambapo ilikuwa ikifanya mazoezi na kupata fursa ya kucheza michezo mitau (3) ya kirafiki.

Katika kambi yake ya wiki mbili Young Africans iliapata fursa ya kucheza michezo mitatu ya kirafiki na timu za Arminia Bielefeld ya ligi daraja la tatu Ujerumani, Dinzlispor FC ilyopo ligi daraja la kwanza nchini Uturuki na Emmen FC iliyopo ligi daraja la kwanza nchini Uholanzai.

Akiongelea michezo ya kirafiki mitatu waliocheza na timu za Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen Fc kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.

Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za mchezo licha ya Arminia kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.

Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wa washambuliaji ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la ut
ata kisha kupewa penati ya utata pia.

Mchezo wa mwisho dhidi ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza tuliutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokuwa makini washambuliaji wetu walichangia sisi kukosa ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda mlango Yusuph Abdu.
"Tunaushukuru uongozi kwa kukubali kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkaa pamoja kwa muda mrefu huku tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa na hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambo mengi ya msingi ambayo yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa yatakayotukabili" alisema 'Brandts'

Timu itaondoka Antalya majira ya saa 9:30 mchana na kufika katika mji wa Instabul majira ya saa 10:50 jioni , kisha baadae majira ya saa 1 na robo usiku itaanza safari ya kuelekea Dar es salaam ambapo inatazamiwa kufika uwanja wa ndege wa kimataifa JNIA jumatatu majira ya saa 10 kasoro alfajiri.

Msafara utakua na jumla ya watu 33, wachezaji 27, na viongozi 6

No comments:

Post a Comment