Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, January 20, 2013

AZAM FC KUJIULIZA KWA SOFAPAKA LEO


Wachezaji wa Azam FC wakiwa mazoezi jana jioni kwenye Uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi, Kenya.
Azam FC inaendelea na maandalizi ya siku saba jijini Nairobi, leo watacheza mchezo wake wa pili dhidi ya SOFAPAKA ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyayo.
Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema mechi itakuwa nzuri kwake kutokana timu hizo kucheza mchezo wa aina inayofanana baada ya kuzifundisha timu hizo.
Stewart alisema mechi hiyo muhimu kwake itakuwa na sura tofauti kwa kukutanisha wachezaji walipata mafunzo kupitia kwake, hivyo mbinu na aina nyingine ya mchezo bado SOFAPAKA wanaitumia.
“Nataraji kuona wachezaji wangu wote wakifanya vizuri hasa wa Azam FC, kupambana na timu uliyoifundisha kunakuwa na ugumu, wanaweza kucheza wakifanana kila sehemu hali itakayopunguza idadi ya magoli kwa moja timu hizo” alisema Stewart.
Alisema wachezaji wake wanaonekana kucheza vizuri kipindi hiki, wamezoea hali ya hewa Nairobi hivyo mchezo na SOFAPAKA watakuwa na kila sababu ya kufanya vizuri.
Naye Kocha wa SOFAPAKA David Ouma alisema kukutana na Azam FC katika mechi ya kirafiki ilikuwa moja ya mipango yao, wanatajia kucheza mchezo wa ushindani zaidi na kuwapa nafasi wachezaji wake wapya walisajiliwa hivi karibuni.
“Haya ni maandalizi mazuri kwa timu yangu, tumeanza mazoezi wiki mbili zimepata, kupitia mechi hii tutajua maendeleo ya timu, wachezaji hasa hawa tuliowasajili, pia tutazidi kujenga urafiki mzuri na Azam FC” alisema kocha Ouma.
Azam FC baada ya mchezo huo, siku ya Jumatatu itapumzika kwa kufanya mazoezi, na kumaliza mchezo wake wa tatu siku ya Jumanne dhidi ya K.C.B utakaochezwa kwenye Uwanja wa City uliopo jijini hapa.
Timu hiyo inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania mzunguko wa mwisho wa ligi utakaoanza Jan 26 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment