WANAMICHEZO 45 wamechukua fomu
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu.
Nafasi zinazowaniwa ni Rais,
Makamu wa Rais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda 13
tofauti.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema waombaji
wapya 11 ambao ni Richard Rukambura anayeomba urais wakati kwa upande wa ujumbe
wa Kamati ya Utendaji ni Kaliro Samson, Jumbe Magati, Richard Rukambura, Omari
Walii, Ahmed Mgoyi, John Kiteve, Stanley Lugenge, Francis Ndulane, Riziki Majara
na Hassan Othuman Hassanoo.
Alisema mwisho wa kuchukua fomu
kwa waombaji wote ni leo (Januari 18 mwaka huu) saa 10 kamili alasiri.
“Orodha kamili ya waombaji ni Athuman
Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Walioomba
kuwania nafasi ya Makamu wa Rais ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace
Karia.
“Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni
Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona,
Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na
Mwanza,” alisema.
Wengine ni Epaphra Swai na Mbasha Matutu
(Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na
Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo,
Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James
Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na
Ruvuma).
Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani
Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida),
Farid Nahdi, Geofrey Nyange, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majara na Twahili
Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa
na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari
Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
No comments:
Post a Comment