Kenedy Mwaisabula aliyeshika mic |
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Waliku wa Mpira wa Miguu (TAFCA) imetangaza matokeo ya usaili wa wagombea uongozi chama hicho, ikiwa imepitisha wagombea sita sita na kuwaengua wagombea watano kwenye nafasi tofauti.
Baada ya usaili wa wagombea hao, Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA iliwaengua wagombea hao watano kwa kutokidhimasharti ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya TAFCA na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na pia kutokidhi utashi wa masharti ya 11 (1) ya kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Katika nafasi ya mwenyekiti Oscar Don Korosso alipitishwa kuwa mgombea pekee baada ya Kenedy Mwaisabula na Jamhuri Kihwelo kuenguliwa kwa kutokidhi masharti ya ibara ya 26 (2) ya Katiba ya TAFCA na kanuni ya tisa ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Katika nafasi ya makamu mwenhyekiti, Kamati imempitisha Lister J. Manyara kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo huku Marco Bundara akipitishwa kuwa mgombea pekee wa nafasi ya katibu mkuu wa TAFCA.
Hali kadhalika wagombea wawili wa nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF, Wilfred Kidau na Magoma Rugora wamekidhi masharti ya Katiba ya TAFCA na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na hivyo watachuana kuwania kura za wajumbe wa mkutano mkuu, huku Ally A Mtumwa akienguliwa kwa kutokidhi masharti ya kanuni ya 11 (1) ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Katika nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wagombea wote wawili, Abubakar Balingula na Aboubakar Salum wameenguliwa kwa kutokidhi masharti ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya TAFCA na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
No comments:
Post a Comment