BAADA ya kuwa 'juu ya mawe' kwa muda
mrefu, bendi ya muziki wa dansi ya Vijana Jazz, 'Wana Air Pambamoto'
imeibuka upya kuanza kupiga muziki kwenye kumbi za starehe, huku ikiwa
imepua vibao viwili vipya kusuuza nyoyo za mashaki wake.
Ikipiga kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi
wa Masae Bar, Kawe wilaya ya Kinodoni jijini Dar es salaam, usiku wa
kuamkia leo, bendi hiyo imedhihirisha kwamba mashabiki wake wengi bado
wapo.
Kwenye ukumbi huo unaotazamana na
kilichokuwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packers, Vijana
Jazz ilithihirisha kuwa 'bado wamo', kwa kupiga nyimbo zake za zamani
zikiwemo 'Mary Maria', 'Mwsiho wa mwezi', 'Ngapulila' na 'mawifi',
zilizopigwa enzi za muasisi wa bendi hiyo, marehemu Ahmed Maneti katika
miaka ya 1980.
Nyimbo hizo ziliwafanya mashabiki wa
bendi hiyo, kucheza kwa hamasa kubwa huku baadhi yao wakifuatisha kuimba
samba mba na wanamuziki waliovuokuwa wakiimba jukwaani na wengine
kwenda jukwaani kutuza waimbaji.
Licha ya kuonyesha kuwa bendi hiyo bado
ni mahiri, wanamuziki wa zamani iliobaki nao ni Roshi Mselela, Nuru
Mhina (Baby White) na viongozi wa bendi Abdallah Mgonahazelu (Katibu) na
Saburi Athuman ambaye ni kiongozi wa bendi.
Vibao vibya ambavyo bendi hiyo imeipua
ni 'Utanieleza nini', utunzi wake kiongozi huyo na Kina mama wanaweza
uliotungwa na Mgonahazelu.
Athumani alisema, nyumbo hizo
zimesharekodiwa na hivi karibuni zitaanza kuingizwa sokoni, lakini
akasema bendi yake itafanya hivyo baada ya kuzipiga mara nyingi
majukwaani na kuzoeleka masikioni kwa mashabiki wao.
Alisema wakati kazi ya kuzirekodi nyimbo
hizo kwa ajili ya kusikilizwa, imeshakamilika, sasa bendi ipo katika
jitihada za kuzirekodi katika video ili ziweze kurushwa kwenye vipindi
vya Televisheni na pia kuuzwa kwa mashabiki.
"Tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete
ametutoa juu ya mawe, hivi vyombo mnavyoona ametuwezesha mheshimiwa
Kikwete. Kwa kweli tunamshukuru sana", alisema Mgoma Hazeru wakati kabla
ya bendi hiyo kuanza kuiba wimbo wao mpya wa 'Utanieleza nini'.
Mratibu wa Budurani zote kwenye ukumbi wa Masae, Juma Mbizo, amesema
atakuwa anazitumia kutoa burudani kwa mashabiki. Nyingine ni kama
Msondo Band na FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma'.
No comments:
Post a Comment