Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 20, 2012

MAPRO WA YANGA KUWASILI WIKI HII



NYOTA wa Yanga Haruna Niyonzima na Khamis Kiiza wanatarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa wiki hii ili kujiunga na wenzao katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama.

Akizungumza leo uwanjani hapo Kocha Msaidizi wa timu hiyo fredy Minziro alisema kuwa wachezaji hao walitarajiwa kuwasiri nchini tangu Jumapili iliyopita lakini badala yake wataingi nchini wiki hii.

Kwa upande wake kiungo wa Kimataifa wa Yanga, Niyonzima alipewa mapumziko ya wiki moja kwenda nchini kwao Rwanda baada ya kurejea kutoka katika mashindano ya chalenji yaliyomalizika mapema mwezi huu Kampala Uganda.

Wakati huo huo, Kocha huyo alisema kuwa mazoezi ya timu yake yanampa morali ya kuona kwamba watakuja kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Alisema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakifanya vizuri katika mazoezi jambo ambalo limekuwa likimpa hali ya kuashiria mafanikio katika mechi za mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Minziro alisema kuwa ana amini kuwa timu hiyo itafanya mabadiliko zaidi katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo kutokana na hali wanayoionesha wachezaji hao wakiwa mazoezini.

“Kadri siku zinavyozidi kusogea mbele kuelekea mzunguko wa pili wa ligi wachezaji wangu wamekuwa wakionesha kiwanga kizuri jambo ambalo limekuwa likinipa hali ya kuwa timu itafanya makubwa zaidi kwenye mzunguko wa pili,” alisema Minziro.

No comments:

Post a Comment