NI jambo la kawaida kwa kila mwanadamu kuwa na ndoto zake kuhusu jambo fulani analoliwaza akilini mwake.
Wapo wanaowaza kujenga majumba ya kifahari wakati hali zao zikiwa duni,wapo wanaowatabiria wenzao kufanya makubwa huku wakifahamu fika hawawezi kufanya jambo hilo wanalowatabiria.
Na hii ndivyo inavyoweza kuwa kwa mchezaji wa zamani wa timu ya Liverpool, Alan Hansen ambaye kwa mawazo yake anaona kuwa mchezaji Daniel Agger anaweza kuiongoza timu hiyo hadi ikatwaa ubingwa Kombe la Ligi ya Europa.
Hansen, ambaye amewahi kutwaa ubingwa wa Kombe hilo la Ulaya mara tatu akiwa na timu hiyo ya Liverpool anaamini kuwa beki huyo wa kushoto ana kila aina ya kiwango ambacho kinaweza kumfanya awe beki bora katika klabu hiyo.
Liverpool jana ilikuwa ikisubiri kwa hamu kufahamu ni timu gani itakutana nayo katika hatua ya 32 ya mashindano hayo baada ya kuchezeshwa droo ya kupanga timu iliyokuwa ikichezeshwa jana mjini Nyon, Uswizi.
Hata hivyo Hansen anasema kuwa anavyoamini beki huyo Mdenmark mwenye umri wa miaka 28, na mchezaji mwenzake Martin Skrtel, wataelewana na kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa.
Mscotland huyo anasema: “Ukiangalia katika sehemu ya beki wa kati Liverpool ipo fiti na Daniel ni mmoja wapo wa wachezaji wanaoimarisha sehemu hiyo,"
Anasema kuwa mchezaji huyo anaimiliki vilivyo sehemu hiyo na kwamba unapoangalia kati ya mabeki 10 bora na yeye yumo.
Mchezaji huyo wa zamani anasema licha ya mchezaj huyo kucheza katika nafasi ya beki wa kati, lakini amekuwa akipanda na kushuka jambo ambalo linamfanya aelewane vizuri na Skrtel na anasema kuwa kila mmoja anaelewana vizuri na mwenzake.
“Skrtel ana nguvu na Daniel ni bora uwanjani,”anasema.
Pamoja na kuwa kwa sasa Liverpool inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, mkongwe anasema kuwa kocha wa timu hiyo kwa sasa anahitaji msaada wa kuiwezesha timu hiyo kupata ushindi katika mzunguko wa Ligi Kuu.
Hansen ambaye liigharimu Liverpool pauni 110,000 wakati akijiunga nayo mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ambayo ilipigwa kwenye uwanja wa Anfield ilikuwa ni Septemba 24, 1977 dhidi ya timu ya Derby County ambapo wageni hao walifungwa bao 1-0 lililofungwa na mchezaji Terry McDermott.
Bao la kwanza kwa Hansen lilipatikana mwezi uliofuata wakati wa mechi Kombe la Ulaya mzunguko wa pili iliyopigwa Oktoba 19 ,1977, katika mechi hiyo ya kwanza iliyopigwa tena kwenye uwanja huo wa Anfield kinara huyo ndiye aliyezikitikisa nyavu akiwa wa kwanza dakika ya 14 ya mchezo huo ambao Liverpool iliiadhibu timu kutoka nchi iliyokuwa Ujerumani Mashariki, Dynamo Dresden mabao 5–1.
Na tangu kipindi hicho Hansen alikuwa akipangwa kikosi cha kwanza hadi anaodoka mwaka 1991 akiwa ameichezea timu hiyo mechi
434
Kwa sasa mkongwe huyo ameteuliwa kumsaidia kocha wa sasa wa timu katika kutafuta wachezaji wa kusajili wakati dirisha dogo litakapofunguliwa mapema Januari mwakani.
No comments:
Post a Comment