Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, November 5, 2012

WAKATI TFF IKIUPONGEZA UONGOZI MPYA TANGA ALIYECHAGULIWA KUWA MAKAMU MWEYEKITI AJIUZULU WADHIFA WAKE HAPO HAPO, HUKO RUVUMA BAADA YA NDUMBARO KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI NA KUJIONDOA, MAPUNDA ABWAGWA MBAYA NA SANGA ONE

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) kimepata uongozi mpya katika uchaguzi uliofanyika Novemba 3 mwaka huu.

Viongozi waliochaguliwa ni Said Soud ambaye ni Mwenyekiti, Beatrice Mgaya, Katibu, Khalid Mohamed Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Juma Mgunda Mwakilishi wa Klabu TFF.

Vile vile chama cha Soka mkoa wa Ruvuma (FARU) nao wamepata viongozi wao baada ya uchguzi uliofanyika juzi kwa kuwachangua Sanga One kuwa Mwenyekiti, Katibu Mkuu Ahmad Charles,Katibu msaidizi Ajaba Chitete na Mwakilishi wa vilabu alichaguliwa ni James Mhagama

Pia Shirikisho la Soka nchini TFF limepongeza viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho na inaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TRFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Tanga.

Vile vile uongozi mpya una changamoto nyingi ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu Tanga kwa kuzingatia katiba ya TRFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.

Kamati ya Uchaguzi ya TRFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF zimepongezwa kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa wake.

No comments:

Post a Comment