Kwa Harambee
stars huu ni mchezo wao wa pili kupoteza katika kipindi cha mwezi mmoja
uliopita ambapo mwezi Oktoba ilifungwa mabao 2-1 na Afrika Kusini mchezo
uliofanyika jijini Nairobi.
Hii
leo
Harambee Stars ilikuwa ikiongozwa na mshambuliaji wake Denis Oliech
akisaidiana na wakali kama Ayubu Timbe, Masika Jerry Santo na James
Wakhungu Situma, ambapo
ilikuwa ikicheza mchezo wa kasi na kujiamini zaidi karibu sehemu kubwa
ya
mchezo lakini hata hivyo utulivu wa wachezaji wa Stars uliwasaidia
katika
kuharibu mipango ya Harambee Stars.
Baada
ya mchezo huo kocha wa Taifa Stars Kim Poulsen alikipongeza kikosi
chake kwa kusema wamecheza mchezo mzuri licha ya mazoezi ya muda mfupi.
Amekiri Harambee Stars ni timu nzuri lakini nidhamu ya kimchezo ya vijana wake imesaidia kuweza kuwadhibiti wapinzani wao.
Amesema kuelekea katika michuano ya Challenge atakuwa na muda wa
kutosha wa kufanya maandalizi mazuri zaidi kabla ya kuanza kwa michuano
hiyo ambayo safari hii yatafanyika nchini Uganda.
Kwa
upande wake kocha wa Harambee Henri Michel amesema kikosi chake
kimecheza mchezo mbovu katika mchezo wa leo na kwamba kabla ya michuano
ya Challenge atalazimika kufanya mabadiliko makubwa katika kuimarisha
kikosi hicho.
Taifa Stars baada ya mchezo wa jana itakuwa imebadili jina na sasa kuitwa Kilimanjaro Stars na itaendelea
kuwepo mkoani Mwanza ikiendelea na maandalizi yao kabla ya kuelekea
nchini Uganda tayari kwa michuano ya Kombe la Challenge ambapo Tanzania
Bara itakuwa katika kundi moja pamoja na Burundi, Sudani Kaskazini pamoja na Somalia.
Wachezaji Nasoro Chollo na Aggrey Moris wanatarajiwa kuondoka katika kambi ya timu hiyo leo na kuelekea Zanzibar kujiunga wa wenzao katika kambi ya timu ya Taifa ya Zanzibar inayojiandaa kwa ajili ya michuano ya Challange.
Kikosi cha Stars Kilichoanza dhidi ya Harambee
Stars: Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Amir Maftah,
Shomali Kapombe, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Thomas
Ulimwengu.
No comments:
Post a Comment