Nahodha Miraji Adam akitoa neno kwa niaba ya wachezaji wenzake |
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa Taifa Stars Peter Tino jana usiku aliwakabidhi timu ya Taifa ya vijana waliochini ya miaka 17 "Serengeti boys" bendera na ujumbe mzito.
Tino ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye halfa hiyo aliwaasa wachezaji kucheza kwa kujituma wakijua kuwa nyuma yao kuna watanzania wanawafatilia na ndio maana wamepewa bendera ya taifa kwa sababu wanaiwakilisha nchi.
"Nyie ni jeshi la Tanzania mnakwenda kupigana mkiwa tayari mmeshashinda nyumbani hivyo vyovyote mnatakavyofanyiwa nyie fikirie mchezo tu", alisema Tino.
Pia aliwaambia kwenye mchezo kuna mbinu chafu ambazo zinaweza kutumika ili kuwadhoofisha kisaikolojia ila wasilitilie maanani bali wafikirie mchezo.
"Mchezo wenu ni sawa na mchezo wetu tuliocheza 1980 dhidi ya Zambia na dakika ya 89 mimi niliwanyamazisha Wazambia mbele ya Rais Mugabe baada ya kufunga bao na kufanikiwa kufuzu mataifa ya Afrika, alisema Tino.
Akizungumza na wachezaji Rais wa Shirikisho la Soka nchini Leodgar Chilla Tenga aliwaasa wachezaji wakazingatie kile tu walichofundishwa na kocha kwani anajua mchezo huu utakuwa mgumu
Timu iliondoka na ndege ya shirika la ndege la Kenya na msafara wa watu 27, wachezaji 18 na viongozi tisa huku wakiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya mchezo wa awali uliochezwa nchini kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kocha wa timu hiyo, Jacob Michelsen alisema kuwa anajua nakwenda kucheza natimu bora ila wao ni bora pia kwani wana faida ya bao la nyumbani.
"Wachezaji wapo kamili na wana ari ya kushinda mchezo huo na kwa sababu nyumbani tulishinda tunaamini tutashinda pia", alisema Jacob
Serengeti boys ambayo imeundwa na wachezaji chipukizi waliopatokana kutokana na mashindano ya Copa Cocacola wanatamani kushinda mchezo ili waweze kuandika historia ambayo haijawahi kuandikwa hapa nchini.
Serengeti boys wamefika hatua hii baada ya kufuzu hatua ya kwanza baada ya Kenya kujiondoa na hatua pili Misri kujitoa pia
LENZI YA MICHEZO tunawatakia kila la heri mfanikiwe kufuzu fainali za vijana zinazotarajiwa kuchezwa nchini Morocco, Machi mwakani
No comments:
Post a Comment