Wagombea
sita wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu wa
Wanawake Tanzania (TWFA) wamewekewa pingamizi na wadau wa mchezo huo.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala,
wagombea hao ni Joan Minja anayewania nafasi ya Mwenyekiti ambaye
amewekwa pingamizi na wadau sita. Pia Isabellah Kapera ambaye anagombea
uenyekiti amewekewa pingamizi moja.
Wagombea
watatu wa nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) nao wamewekewa pingamizi. Wagombea hao ni Julliet
Mndeme (pingamizi sita), Zena Chande (pingamizi nne) na Jasmin Soud
mwenye pingamizi tatu.
Naye Rahim Maguza anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji amewekewa pingamizi moja.
Licha
ya pingamizi hizo, wagombea wote wanatakiwa kuhudhuria usaili wakiwa na
vyeti vyao halisi vya kitaaluma utakaofanyika Oktoba 12, 13 na 14 mwaka
huu kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
Salaam kuanzia saa 3 asubuhi.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment